Home LOCAL WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA MAJI WA NGULYATI BARIADI

WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA MAJI WA NGULYATI BARIADI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Leo 25 Machi 2023, amezindua mradi wa maji wa Ngulyati – Nyamswa Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu pamoja na kukabidhi mitambo ya kuchimba visima virefu vijijini iliyotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita.

Mradi huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.3 utatoa huduma kwa wananchi 10,106 wa vijiji vya Ngulyati, Nyamswa na Nyasosi.

Mradi huo umeanza kutoa huduma una uwezo wa kuzalisha maji lita 15,800 kwa saa sawa na lita 284,000 kwa siku.

Akitoa Taarifa ya Mradi huo Meneja wa RUWASA Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Mariam Majala amesema mahitaji ya ya Maji katika vijiji hivyo vitatu ni Lita 271, 900 hivyo uzalishaji wa maji katika mradi huo unajitosheleza.

Akizungumzia mradi huo Waziri Mkuu, amesema mradi huo ni muendelezo wa kampeni ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani.

Previous articleWAZIRI MKUU AKAGUA MIRADI WILAYA YA ITILIMA
Next articleWAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WILAYA YA BARIADI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here