Home LOCAL WANAHABARI MKOANI MOROGORO WAPAZA SAUTI MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI

WANAHABARI MKOANI MOROGORO WAPAZA SAUTI MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI

NA: FARIDA MANGUBE MOROGORO.
Kuelekea mkutano mkuu wa jukwaa la wahariri nchini (TEF), Wanahabari Mkoani Morogoro wameiomba serikali kuendelea kuondoa  baadhi ya sheria kandamizi ili kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa habari.
Wakizungumzan nje ya mkutano uliondaliwa na kamati tendaji ya TEF wanahabari hao akiwemo Idda Mushi mwandishi wa ITV na mjumbe wa MISA TANZANIA alisema pamoja na Serikali kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha mwenendo wa sekta ya habari unakwenda vinzuri bado kuna haja ya  kuondolewa kwa sheria kandamizi ili  kukuza sekta hiyo.
‘Mazingira ya upatikanaji wa habari kwa sasa ni mazuri, tumeona serikali imeruhusu kuchambuliwa kwa baadhi ya sheria kandamizi zinazozuiya uhuru wa habari, tunaamia yale yote aliyotuahidi ya kuhakikisha maboresho ya sheria zote kandamizi za uhuru wa habari atazifanyia kazi hivyo imani yetu mazingira yatakuwa mazuri zaidi.’ alisema Idda Mushi.
Kwa upande wake Latifa Ganzal mwandishi wa gazeti la Uhuru na Mzalendo Mkoa wa Morogoro aliwataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na maadili ya uandishi wa habari ili kuweka utofauti kati ya mwandishi wa habari na watumiaji wengine wa mitandao.
Naye mratibu wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Thadei Hafigwa alisema kwa sasa kuna ushirikiano mkubwa sana kati ya Jukwaa la wahariri na wadau wa habari hali inayopelekea kuwa na utawi mzuri wa sekta ya habari.
Akizungumza na waandishi wa habari Mjumbe wa kamati tendaji jukwaa la wahariri Tanzania Neville Meena alisema  tayari mabadiliko ya sheria za habari ya 2016 yamewasilishwa bungeni kwaajili ya kuondoa sheria kandamizi za upatikanaji wa taarifa.
Jane Mihanji mjumbe wa kamati tendaji jukwaa la wahariri kwa upande wa wanawake alisema  mikakati iliyopo kwa sasa ili kuhakikisha waandishi wahaari wananwake hawatoeki kwenye sekta hiyo  ni kuwaendeleza kielimu ili wafanye kazi kwa bidiii na kufikia kwenye nafasi za juu kama ilivyo kwa wananume.
Mkutano Mkuu wa jukwaa la wanahariri wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ya taaluma ya habari unatarajiwa kufanyika Machi 29 hadi Machi 31 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri  wa Habari,Mawasiliano na Teknilojia ya Habari Mh.Nape Nnauye. 
Mwisho
 
Previous articleJUMUIYA YA WAZAZI ILALA YAKABIDHI VIFAA VYA SHULE 
Next articleTANZANIA, CUBA KUANZISHA MAENEO MAPYA YA USHIRIKIANO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here