Home LOCAL WAENDESHA MASHTAKA NA WAPELELEZI WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

WAENDESHA MASHTAKA NA WAPELELEZI WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Na Farida Mangube. Morogoro 

WAENDESHA mashtaka na wapelelezi juu ya upelelezi unaofanikisha mshtaka wa kutoka vyombo mbalimbali  wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi wakijua ya kwamba  adui wa kwanza katika kutoa haki ni rushwa.

Naibu Mkuu wa Chuo Mipango , Fedha na Utawala kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto , Profesa  Fatihiya Massawe alisema hayo jana mjini Morogoro wakati akifunga mafunzo yaliyodumu kwa wiki mbili ya upelelezi unaofanikisha uendeshaji wa mashtaka wenye tija ili kuboresha upatikanaji wa haki jinai.

Profesa  Massawe alisema kuwa jukumu la upelelezi  na uendeshaji wa mashtaka ni dhamana waliyopewa kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania.

Hivyo aliwataka kuwajibika kutenda kazi zao kwa mujibu wa sheria , kanuni , taratibu  na miongozo mbalimbali iliyopo, bila kusahau kuweka mbali upendeleo  au chuki katika uwajibikaji wao.

“Niwakumbushe  pia kuwa mfanye kazi zenu vizuri mkijua kuwa adui wa kwanza katika kutoa haki ni rushwa , hivyo muepuke rushwa kwa namna yoyote ile “ alisisitiza Profesa  Massawe

Alisema lengo kuu la mafunzo hayo ni kupunguza na kumaliza kwa asilimia tano  mashauri ya mlundikano yaliyopo Mahakamani yanayochelewa kusikilizwa kutokana na upelelezi kutokamilika kwa wakati ifikapo mwaka 2025.

“Matarajio ya Mahakama ni makubwa juu ya kuongezeka kwa kasi ya kushughulikia mashauri kwa kukamilisha upelelezi kwa wakati  na  mtakuwa mabalozi wazuri kwa wengine ambao  hawajapata bahati ya kuhudhuria mafunzo haya” alisema Profesa  Massawe 

Akizungumzia matumizi ya Tehama , Profesa  Massawe  alisema  kwa hivi sasa hatuwezi kukweka kuitumia , Tehama ni fursa ya maendeleo ambayo  yanawezesha  upatikanaji wa taarifa mbalimbali  .

Profesa  Massawe  alisema kwa mfano , mahakama imewezesha maamuzi ya mahakama , sheria na miongozo mbalimbali kupatikana kwenye mtandao wa Tanzilii ( Tanzania Legal Information Institute).

Profesa  Massawe  alisema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maboresho ya Mahakama ambayo yanatekelezwa kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano 2020/21- 2024/2025  na ni utekelezaji pia wa Sera ya Mafunzo ya Taifa 2003 pamoja na Sera ya Mafunzo ya Kimahakama 2019.

Washiriki 250 kutoka taasisi za Ofisi za Mashtaka,  Jeshi la Polisi,  Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya , Taasisi ya  Kuzuia na Kupambana Rushwa  , Mamlaka ya  Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania  pamoja na Ofisi ya Kudhibiti Fedha Haramu  ambao walipatiwa mafunzo hayo kwa awamu  nne .

Mafunzo hayo yalifunguliwa na Jaji Mfawidhi  wa Mahakama  Kuu ya Tanzania , Kanda ya Morogoro,  Paul Ngwembe ,  Februari 27, mwaka huu  katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Morogoro  na yaliandaliwa na Mahakama ya Tanzania  na kuendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa ufadhili wa Banki ya Dunia kupitia mradi wa  Maboresho awamu ya pili.

Katika risala ya wahitimu  iliyosomwa kwa niaba yao na Wakili wa Serikali Ofisi ya Taifa ya Mashtaka , Sara Amandus, aliishukuru  Mahakama ya Tanzania kupitia Chuo cha Uongozi wa Mahakama kwa kutoa  mafunzo hayo  yaliyowajengea   uelewa wa pamoja kwenye sheria , mbinu  na taratibu za upelelezi na uendeshaji wa mashtaka

Pia mafunzo hayo  yametoa fursa kwao kubalilishana uzoefu kuhusu utendaji kazo wao wa kila siku ikiwemo changamoto zinazotokana na kukua kwa teknolojia  na kubadilika kwa mbinu za uhalifu na wahalifu.

Mwisho.

Previous articleMBUNGE ZUNGU AWATAKA WADAU WA SAMAKI KUACHA UVUVI HARAM
Next articleTANROADS IMEWATAKA WATUMISHI WAKE KUTENGA MUDA WA MAZOEZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here