Home BUSINESS WADAU WA GESI KUTOKA NCHI ZAIDI YA 30 KUKUTANA KATIKA KONGAMANO KUBWA...

WADAU WA GESI KUTOKA NCHI ZAIDI YA 30 KUKUTANA KATIKA KONGAMANO KUBWA JIJINI DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania LPG Association, Amos Mwansumbue (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa kutangaza maonesho ya gesi ya kupikia (LPG EXPO Afrika Mashariki 2023) yanayotarajiwa kufanyika tarehe 15 hadi 16 mwezi huu kwenye hotel ya  Rotana jijini Dar es salaam. Kulia ni Catherine Ho, Mkurugenzi Mkuu wa LPG EXPO ambao ndio waandaaji wa maonesho hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa LPG EXPO,Catherine Ho akizungumza.
Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.

Waziri wa Nishati, January Makamba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Wadau wa Gesi ya LPG Afrika Mashariki 2023 ambalo litawaleta wadau mbalimbali kutoka nchi zaidi ya 30 ambao watashiriki katika mkutano na maonesho maalum tarehe 15 hadi 16 Machi, mwaka huu.

Akizungumzia Kongamano hilo Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha wadau wanaohusika na biashara ya gesi ya kupikia majumbani (LPG), Amos Mwansumbue amesema kuwa Katika kongamano hilo, wadau wa ndani na nje ya nchi watakutana kuzungumzia masuala mbalimbali yanayoikabili sekta hiyo katika kanda ya Afrika Mashariki, kuonyesha bidhaa zao, kuchochea uwekezaji pamoja na mahusiano mazuri.

Aidha, ndani ya kongamano hili, Oryx Energies itaendeleza jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kudhamini Warsha ya WLPGA Good Industry Practices and Cooking For Life itakayofanyika tarehe 14 Machi. Washiriki wa warsha hii watapata fursa ya kufahamu mipango ya matumizi ya gesi ya LPG nchini Tanzania na mikakati mbalimbali ya kukabiliana na vikwazo vikuu vinavyokwamisha safari kuelekea matumizi ya nishati safi na salama zaidi ya kupikia.
Likiwa na wazungumzaji wenye weledi pamoja, majopo ya majadiliano na bidhaa na huduma mbalimbali kwenye maonesho, Kongamano la Wadau wa Gesi ya LPG Afrika Mashariki – Tanzania 2023 ni fursa nzuri ya kupanua uelewa na kupata ufumbuzi kwa wadau wa biashara katika sekta hii.
Kwa taarifa zaidi na kwa ajili ya kujisajili tembelea https://lpgexpo.com.sg/ info@lpgexpo.com.sg

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here