Home LOCAL UTALII 255 COMMUNITY KUITANGAZA SEKTA YA UTALII NDANI 

UTALII 255 COMMUNITY KUITANGAZA SEKTA YA UTALII NDANI 

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa kaskazini Unguja Angelina Malembeka akigawa mabeki ya shule na vifaa vyake Kwa Watoto wa mahitaji maalum wa shule ya Mama Afrika katika ziara mbuga ya Hifadhi ya Mikumi.

Wanafunzi wa mahitaji Maalum wa shule ya Mama Afrika wakiwa katika Picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Utalii 255 Community Angelina Malembeka mara baada kupewa mabegi na vifaa vya Shule

Na: Heri Shaaban (Mikumi)

TAASISI ya Utalii 255 Community imejipanga kutangaza Sekta ya Utalii kwa kutangaza Utalii wa ndani kuunga Mkono Juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutangaza vivutio vya Nchi yetu .

Hayo yalisemwa na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Utalii 255 Community Siza Mazongera wakati wa ziara ya Watoto wenye mahitaji maalum wa Shule ya Mama Afrika walitembelea Hifadhi ya Mbunga ya Mikumi iliyopo mkoani Morogoro katika ziara iliyoandaliwà na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kaskasini Unguja Angelina Malembeka ambaye pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Utalii Community chini ya ufadhili wa Benki ya CRDB .

“Dhumuni la Taasisi yetu ya Utalii 255 Community kutangaza utalii wa ndani katika mbuga zetu na vivutio mbalimbali zilizopo hapa nchini katika kukuza sekta ya Utalii” alisema Siza .

Makamu Mwenyekiti. Siza Mazongera alisema Taasisi ya Utalii 255 ilianzishwa Mwaka 2019 ambapo ilizinduliwa na Mke wa Rais Mstaafu Mama Salima Kikwete, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Angelina Malembeka.

Siza Mazongera alisema ni vyema Wananchi watembelee mbuga zetu na vivutio vya ndani waweze kuongeza pato la Taifa.

Mwenyekiti wa Utalii 255 Community ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Kaskasini Unguja Angelina Malembeka alisema, CRDB imechangia katika ufadhiliwa watoto hao wenye Mahitaji Maalum.

Mbunge Malembeka alitaja vifaa alivyogawa kwa watoto hao ni madaftari, mabegi, kalamu, seti ya vifaa vya hesabu pamoja na kuwafungulia akaunti za akuba katika Benki ya CRDB .

Mratibu wa safari ya Utalii255 Community, Hatibu Baruti alisema wameandaa ziara ya Watoto hao katika Mbuga ya Hifadhi ya Mikumi wakajionee na kujifunza kwa vitendo kwani Watoto hao wenye mzhitaji Maalum ni wanahitaji kupata faraja kama watoto wengine .

Hatibu alisema safari za Utalii katika Hifadhi ni endelevu na Mikakati ya taasisi hiyo kutoa vijarida kuielezea sekta ya utalii wa nchi yetu .

Mwongoza Utalii wa Mbuga ya Taifa ya Mikumi James Aloni, aliwataka Wananchi kutembelea katika Mbuga hiyo kujifunza mambo mbalimbali.

Alisema mbuga hiyo ilianzishwa Mwaka 1964 ina ukubwa wa eneo kwa sasa Ekali 3230, awali zilikuwa hekari 11700 .

Mkurugenzi wa shule ya Mama Afrika iliyopo Zanzibar Lucy Mpembo, alimpongeza Mbunge wa Viti Maalum . Angelina Malembeka kwa ziara hiyo ya mafunzo na Wanafunzi wake wamejionea Vitu vingi vya Utalii Kwa vitendo .

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here