Home BUSINESS TWCC, giZ WASHIRIKIANA KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI KUPITIA MRADI WA (WE4A)

TWCC, giZ WASHIRIKIANA KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI KUPITIA MRADI WA (WE4A)

Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma hamza akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Mjasieiamali  Mwanamke Afrika iliyofanyika leo Machi 10, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Kiongozi msaidizi wa Mradi wa E4D kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani GiZ Denis Bangula akizungumzia utekelezaji wa mradi huo katika hafla hiyo Jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Bodi ya TWCC ambaye pia ni Mgeni rasmi katika hafla hiyo Victoria Mwanukuzi akizungumza alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuhitimishwa kwa hafla hiyo iliyofanyika leo Machi 10, 2023 Mlimani City Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma hamza (kushoto) akiongoza mdahalo maalumu uliowashirikisha baadhi ya wajasiriamali walionufaika na Mradi wa kuwaendeleza Wanawake Wajasiriamali (WE4A).

Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma hamza (kulia) akijadiliana jambo na Mgeni rasmi wa hafla hiyo Victoria Mwanukuzi (katikati) wakati wa hafla hiyo.

Baadhi ya washiriki waliohudhuria kwenye  hafla hiyo.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR.

Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (giZ)  wameadhimisha siku ya Majasiriamali Mwanamke Afrika ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofikiwa kilele chake Machi 8 mwaka huu.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo Machi 10, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza amesema kuwa  lengo la maadhimisho hayo ni kuwapongeza Wajasiriamali hao na kutambua mchango wao katika kazi zao za Ujasiriamali.

Amesema kuwa TWCC imekuwa ikiandaa matukio mbalimbali kutambua mchango wa wanawake katika Biashara sambamba na kutoa tuzo kwa wanawake wanazofanya vizuri kwenye Biashara.

“TWCC tumekuwa tukiandaa matukio kama haya kila mwaka lengo likiwa kuendelea kutambua mchango wa Wajasiriamali katika kazi zao na kuwahamasisha ili kufanya vizuri zaidi” amesema.

Aidha amesema tukio hilo limekuwa na mafanikio makubwa kutokana na Ushirikiano mkubwa wa Shirika la giZ kupitia Programu inayowaendeleza Wanawake Wajasiriamali kupitia mradi wa (WE4A) unaotekelezwa hapa nchini kwa ufadhili wa Shirika la giZ kupitia TWCC.

Kwa upande wake Kiongozi msaidizi wa Mradi wa (E4D) unaosimamiwa na kutekelezwa na Shirika la giZ Denis Bangula amewataka Wajasiriamali Wanawake hapa nchini kuchangamkia fursa hiyo ukizingatia kuna idadi ndogo ya Wajasiriamali wanaonufaika na mradi huo ukilinganisha na nchi nyingine katika Bara la Afrika.

“Tanzania kuna Wajasiriamali 41 tu waliojiunga na Programu hii tofauti na nchi nyingine ikiwemo Kenya yenye Wajasiriamali zaidi ya 200. Hivyo niwasihi Wajasiriamali kushiriki kwa wingi kwenye programu hii Ili kuweza kufikia malengo yenu” amesema Bw. Bangula na kuongeza kuwa.

“Mradi huu unalenga kuwahusisha zaidi wanawake kushiriki katika uchumi wa Taifa kwa kuongeza ajira kwa vijana kupitia Biashara wanazozifanya na kuwasaidia Wajasiriamali ili kuweza kuchangia katika pato la Taifa. ameongeza.

Aidha ameahidi kuendelea kushirikiana na TWCC kwa kufanyakazi kwa pamoja katika miradi inayofuata inayolenga kuwajengea uwezo wajasiriamali na kuimarisha Biashara zao.

Naye mjumbe wa bodi ya TWCC ambaye pia ni mgeni rasmi katika hafla hiyo Bi. Victoria Mwanukuzi amesema kuwa zipo changamoto zinazowakabili Wajasiriamali likiwemo suala la masoko vifungashio na mitaji na kwamba, TWCC imekuwa ikizifanyia kazi changamoto hizo kwa kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi kwa kuwatafutia fursa mbalimbali zikiwemo masoko ya kuuzia bidhaa zao ndani na nje ya nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here