Home LOCAL TCU, IUCEA YAWALETA PAMOJA WADAU WA ELIMU YA JUU NCHI ZA AFRIKA...

TCU, IUCEA YAWALETA PAMOJA WADAU WA ELIMU YA JUU NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI JIJINI DAR

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza alipokuwa akifungua rasmi Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Wanataaluma, Sekta ya Umma na Sekta Binafsi lilioandaliwa na Barasa la Vyuo Vikuu Afrika mashariki kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika Kituo cha Mikutano ya cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JKNCC) kuanzai leo tarehe 15hadi 17, Machi 2023.

Mwenyekiti wa Barasa la Vyuo Vikuu Afrika mashariki, Prof. Gaspard Banyankimbona akielezea madhumuni ya Mkutano huo alipokuwa akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo unaofanyika kwa siku tatu Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa akizungumza katika Mkutano huo alipokuwa akiwatambulisha na kuwakaribisha wazungumzaji mbalimbali katika mkutano huo.

Mwakilishi kutoka Serikali ya Ujerumani ambaye pia ni Mkuu wa Ushirikiano wa Kikanda katika Balozi wa Ujerumani Bw. Johannes Fechter akizungumza katika Mkutano huo uliodhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (giZ).

Mkurugenzi wa Sekta za Jamii Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Irene Isaka, akizungumza wakati wa kongamano hilo.

Wadau mbalimbali waliohudhuria kwenye mkutano huo wakifuatilia Hotuba ya mgeni rasmi pamoja na wazungumzaji wengine waliozungumza katika mkutano huo.

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO).

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewataka wadau wa Elimu ya Juu katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza ushirikiano kwa kutanua wigo wa huduma wanazotoa kwa kufungua mipaka ya elimu ndani na nje ya Afrika Mashariki ili kuleta tija ya ajira katika jumuiya hiyo.

Amesema kuwa ili kufanikisha hilo juhudi za makusudi zinahitajika kwa kushirikiana na Sekta Binafsi ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha uchumi wa nchi hizo kwa kuzalisha ajira katika sekta mbalimbali.

Waziri Mkenda ameyasema hayo leo Machi 15, 2023 wakati akifungua Mkutano wa 12 wa Sekta ya Elimu ya Juu ulioandaliwa na Barasa la Vyuo Vikuu Afrika mashariki kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) unaofanyika kwa siku tatu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JKNCC) kuanzai leo tarehe 15 hadi 17, Machi 2023.

“Katika kulifanikisha hili ni visuri sasa Mawaziri wa elimu wa Jumuiya ya Afrika mashariki tupate fursa ya kukaa pamoja chini ya Baraza la Vyuo vikuu Afrika Mashariki tuone tunaweza kufanya nini” amesema Prof. Mkenda na kuongeza kuwa.

“Vile vile tunahitaji kushirikisha Sekta Binafsi ambayo zitaweza kutoa msaada kwa wanafunzi kama mikopo ambayo mwanafunzi ndani ya jumuiya anaweza kunufaika nayo akitoka nchi moja kwenda nyingine ndani ya jumuiya yetu” ameongeza.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa amesema lengo hasa la Jukwaa hilo ni kuwakutanisha wanataaluma, Sekta ya Umma pamoja na Sekta Binafsi katika mashirikiano, na kuangalia namna ya kukuza mashirikiano katika sekta mbalimbali ili kuleta tija ya elimu inayotolewa katika taasisi za elimu ya juu.

“Katika Mkutano huu wamealikwa wenye viwanda wapo hapa, Waajiri pamoja na Sekta Biafsi. Pia kuna maonesho yanaendelea hapa, kwa hiyo hii ni fursa kubwa ya wao kujadiliana na kuona ni maeneo gani ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho hasa katika ile mitaala ambayo inatoa vijana wetu ili nao wanapotoka waweze kuwa na ujuzi ili waweze kwenda kuchukua fursa za ajira, lakini pia kuweza kujiajiri wenyewe” amesema Prof. Kihampa.

Amesema anaamini  kuwa hiyo ni fursa nzuri kutokana  na uwepo wa wadau hao ambao wanakwenda kukutana na wanataaluma wanaotoa elimu kwa vijana wanaosoma katika taasisi zao.

Naye Mwenyekiti wa Barasa la Vyuo Vikuu Afrika mashariki, Prof. Gaspard Banyankimbona amesema kuwa mkutano huo utajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili taasisi za Elimuya Juu na kuzipatia ufumbuzi na kwamba anamiini kuwa ushiriki wa Sekta Binafsi utawezesha upatikanaji wa suluhisho la baadhi ya changamoto hizo likiwemo suala la ajira kwa wahitimu wanaotoka katika vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu Afrika Mashariki.

Mkutano huo wa siku tatu umehudhuriwa na wadau takribani 180 kutoka katika nchi za Jumuiya ya Afrika Nashariki na unatarajiwa kufikia tamati siku ya Ijumaa Machi 17, Mwaka huu.

Picha mbalimbali za Mwenyekiti wa Barasa la Vyuo Vikuu Afrika mashariki, Prof. Gaspard Banyankimbona, na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa wakiwa katika Banda la TCU walipokuwa wakitembelea mabanda ya Vyuo Vikuu na Taasisi mbalimbali za Elimu ya Juu wakati wa Mkutano huo.

Previous articleKAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA UTEKELEZAJI MIRADI YA AFYA RRH-IRINGA
Next articleRAIS MHE. SAMIA AWASILI JIJINI PRETORIA KWAAJILI YA ZIARA YA KISERIKALI YA SIKU MOJA NCHINI AFRIKA KUSINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here