Home BUSINESS TAARIFA KWA UMMA – BENKI KUU YA TANZANIA YAONGEZA MUDA WA USIMAMIZI...

TAARIFA KWA UMMA – BENKI KUU YA TANZANIA YAONGEZA MUDA WA USIMAMIZI WA YETU MICROFINANCE BANK PLC

Itakumbukwa kwamba, kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha sheria  namba 56(1)(g)(iii) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006,  Benki Kuu ya Tanzania iliamua kuchukua usimamizi wa Yetu Microfinance Bank  Plc kuanzia tarehe 12 Disemba 2022 baada ya kubaini kuwa ilikuwa na upungufu  mkubwa wa ukwasi na mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya Mabenki na  Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.  

Baada ya kuchukua usimamizi wa benki hii, Benki Kuu ya Tanzania ilisitisha  shughuli za utoaji wa huduma za kibenki za Yetu Microfinance Bank Plc kwa  muda wa siku tisini ili kuipa nafasi Benki Kuu ya Tanzania kutathmini hatua za  kuchukua ili kupata ufumbuzi wa suala hili. Benki Kuu ya Tanzania inapenda  kuuarifu umma kuwa mchakato wa kutathmini hatua za kuchukua ili kupata  ufumbuzi wa matatizo ya Yetu Microfinanc Bank Plc haujakamilika hivyo muda  wa usimamizi umeongezwa kwa kipindi cha siku thelathini (30) kuanzia tarehe 12 Machi 2023.  

Benki Kuu ya Tanzania inauhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya  wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya  fedha.  

GAVANA 

BENKI KUU YA TANZANIA

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 14,2023
Next articleASANTENI KWA KUSHIRIKIANA NASI KATIKA KUBORESHA SEKTA YA AFYA- DKT. MOLLEL
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here