Home Uncategorized STAMICO YAUNGANA NA WANAWAKE DUNIANI KUSHEREHEKEA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI

STAMICO YAUNGANA NA WANAWAKE DUNIANI KUSHEREHEKEA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI

Wafanyakazi Wanawake wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wameungana na Wanawake wengine Duniani katika kuadhimisha siku ya Mwanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa Jijini Dar es Salaam.

Katika maadhimisho hayo Wanawake kutoka STAMICO walijumuika na wenzao kutoka katika taasisi nyingine kushiriki maandamano maalum yaliyoanzia Mtaa wa Lumumba kuelekea kwenye viwanja vya Mnazi mmoja na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Wanawake wa STAMICO, Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi wa Taasisi hiyo Bi Leah Jeriko amesema kuwa maadhimisho hayo yamekuwa ni fursa kubwa kwao kukutana na Wanawake wenzao na kwamba wametumia maonesho kutangaza bidhaa ya mkaa mbadala unaotokana na mabaki ya mkaa wa mawe ‘Rafiki Briquettes’

“STAMICO imeshiriki maadhimisho haya kufurahia Siku hii ya Mwanawake Duniani na wenzetu lakini pia tukitangaza bidhaa yetu ya mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes tukiwaambia wakina mama ubora wa mkaa huu na faida zake” amesema Leah

Nao Baadhi ya Wanawake kutoka katika Shirika Hilo kwa nyakati tofauti wameshindwa kuzuia furaha zao Kufuatia ushiriki wao kwenye maadhimisho hayo na kusema kuwa itaongeza hamasa katika kitekeleza majukumu yao.

STAMICO imeshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo wanawake katika ofisi zote za makao makuu Dodoma, Dar es Salaam na Ofisi ya Kiwira Songwe wamejumuika kusheherekea. Kaulimbiu ya mwaka huu umebebwa na ujumbe usemayo, “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia: Chachu Katika Kuleta Usawa wa Kijinsia”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here