Timu ya Simba SC imefanikiwa kusogea hadi nafasi ya pili ya Kundi C kufuatia kuichapa timu ya Vipers goli 1-0 katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika uliopigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Goli la Simba lilifungwa na kiungo mshambuliaji Clatus Chama katika dakika ya 45 Kipindi cha kwanza, goli lililowapeleka mapumziko katika mchezo huo.
Kipindi cha pili timu zote zilirudi uwanjani na kucheza kwa kasi huku kila timu ikifanya mabadiliko, ambapo kwa upande wa Simba walimpumzisha Patrick Phil na nafasi yake kuchukuliwa na Jian Baleke, na Pape Sakho alipumzika kumpisha Peter Banda ambapo mabadiliko hayo yaliiwezesha Simba kuongeza nidhamu katika mchezo huo.
Hadi mwamuzi wa mchezo huo anapuliza filimbi ya mwisho kumaliza mchezo huo, Simba imetoka kifua mbele kwa kuchukua alama tatu muhimu.
Kufuatia matokeo hayo timu ya Simba inapanda hadi nafasi ya 2 ya msimamo wa Kundi lao na alama 6 nyuma ya Raja Casablanca yenye alama 12 baada ya kuichapa timu ya Holoya yenye alama 4 akishika nafasi ya 3 huku Vipers ikishika mkia wa kundi hilo kwa kuwa na alama 1 pekee