Na: Tima Sultan , DAR ES SALAAMÂ
SHABIKI na Mwanachama wa Klabu ya Simba, Michael Charles Magige, amewataka Horoya FC kuwasamehe kwani lazima leo wata waharibia malengo yao kwakuwafunga kwenye Uwanja wa Mkapa nakuweka Historia nyingine ya kuingia hatua ya Robo fainali michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.
Simba leo saa 1:00 usiku wanatarajia kushuka kwenye Dimba hilo na kupepetuana na Kikosi hicho cha Horoya kutoka nchini Guinea kuitafuta tiketi ya kuingia robofainali kwenye mashindano hayo ya kimataifa.
Magige ni mwanachama hai wa Tawi la Simba Plutnum lililopo Teme, Jijini Dar es Salaam, ameyazungumza hayo akiwa uwanjani hapo akisubiria mchezo wao uanze.
Amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu Kwa kumfikisha siku ya leo
kuweza kuwa sehemu ya mashuhuda wa historia ambayo muda sio mrefu inaenda kuwekwa na timu yake pendwa
Simba Sport Club.
Michael amesema anaiamini mno n timu yake kuw wana wachezaji wazuri ambao wameamua kucheza kwa faida ya timu basi wapinzani wao Horoya hawana budi kuwasamahe nilazima waingie robo fainali.
“Ninawaamini sana wachezaji wangu ninaamini pia kwa viongozi wangu wa klabu pia ninaamini na Mashabiki wenzangu wanachama na wale wote wenye kuitakia Mema timu yetu pendwa ki mtazamo mchezo utakuwa mgumu sana kwa kuwa ni wa kuamua hatma ya nani aende Robo Fainali,” alisema