Home LOCAL SENYAMULE AHIMIZI BALOZI KUJENGA DODOMA

SENYAMULE AHIMIZI BALOZI KUJENGA DODOMA

Ameyasema hayo leo tarehe 28/02/2023 mara baada ya kukutana na balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Elisabeth Jacobsen aliembatana na ujumbe wake katika ziara ya kikazi ya siku mbili ya kutembelea Mkoa wa Dodoma.
Mhe. Senyamule amemshukuru Balozi wa Norway kwa kutembelea Dodoma, kuona fursa za uwekezaji na kuimarisha ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili pia hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika kuifaharisha Dodoma.
“Tunawakaribisha sana Dodoma, makao makuu ya nchi yetu, viwanja 67 vimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi na makazi ya balozi mbalimbali” Senyamule alisisitiza.
Ameongeza kwa kusema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati ili Dodoma iweze kufunguka kimataifa.
Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja ujenzi wa barabara za mzunguko, ndani na nje ya Mkoa pamoja na ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato.
Naye Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen amesema kwa miaka mitano aliyokaa Tanzania ameshuhudia mageuzi na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ambayo yamefanyika katika kipindi kifupi na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo agenda ya maendeleo endelevu.
Amesema kwa kipindi cha miaka miwili Mkoa wa Dodoma umebadilika sana kutokana na uwekezaji uliofanyika katika sekta ya miundombinu, Elimu, Afya na mazingira ya uwekezaji ikiwa ni pamoja ujenzi wa mji wa Serikali.
Balozi Elisabeth katika ziara yake ameambatana na ujumbe wa watu 21 na wanatembelea Mji wa Serikali Mtumba, Hospitali ya Benjamin Mpaka, Ujenzi wa Reli ya Kisasa na ujenzi wa ndege wa Msalato.
Aidha, Mratibu wa kikosi kazi cha Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe amesema ujio wa Balozi wa Norway ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali kuhamia Dodoma hususani kuhamasisha ujenzi wa ofisi za ubalozi na mashirika ya kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akimpatia zawadi Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Elisabeth Jacobsen aliembatana na ujumbe wake mara baada ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa ziara ya kikazi ya siku mbili. Balozi Elisabeth na ujumbe wake watatembelea Mji wa Serikali Mtumba, Hospitali ya Benjamini Mkapa na Chuo Kikuu cha Dodoma.
Previous articleKATIBU MKUU DKT. YONAZI APOKELEWA RASMI OFISI YA WAZIRI MKUU AOMBA USHIRIKIANO
Next articleNHIF YAKABIDHI MAJINA YA WALIMU WALIOGHUSHI NYARAKA KWA TUME
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here