Home LOCAL RC MNDEME APOKEA MTAMBO WA KISASA WA KUCHIMBA VISIMA VIREFU VYA MAJI...

RC MNDEME APOKEA MTAMBO WA KISASA WA KUCHIMBA VISIMA VIREFU VYA MAJI SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (aliyevaa suti nyeusi) akikata utepe wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa KASHWASA, John Zengo akifuatiwa na Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amepokea Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji ambao ni sehemu ya mitambo 25 ya kuchimba visima vya maji iliyonunuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maji kwa Fedha za UVIKO – 19.
 
Mtambo huo wenye uwezo wa kuchimba kisima hadi mita 300 umepokelewa leo Jumatatu Machi 27,2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
 
Akizungumza wakati wa kupokea mtambo huo wa kisasa wa kuchimbia visima virefu kwa niaba ya wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameagiza mtambo huo utunzwe na utumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
 
“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kununua mtambo huu wa kuchimbia visima virefu vya maji. Mhe. Rais Samia amedhamiria kuwapatia wananchi huduma ya maji safi na salama lakini pia kumtua mama ndoo kichwani….Nasi Shinyanga tunasema ‘Dkt. Samia Maji Safi na Salama Bombani, Maji nyumbani, Kazi Iendelee’”, amesema Mhe. Mndeme.
 
“RUWASA nendeni mkafanye kazi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama na mhakikishe pia kabla ya kuanza kuchimba muwe mmefanya utafiti kuwa na uhakika kama kweli maji yapo”,ameongeza Mkuu huyo wa Mkoa.
 
Aidha amewataka wananchi kulinda vyanzo vya maji na miundombinu ya maji ili miradi ya maji inayojengwa idumu huku akibainisha kuwa serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji.

Muonekano wa sehemu ya Mtambo wa Kisasa wa kuchimba visima virefu vya maji 

Akitoa taarifa ya Mapokezi ya mtambo wa kisasa wa uchimbaji visima, Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela amesema kwa kuanzia, uchimbaji visima virefu utaanza mara moja katika vijiji vinne ambavyo ni Itilima na Mwashinogela katika wilaya ya Kishapu na Ubagwe na Kinamapula katika Halmashauri ya Ushetu.
“Mkoa wa Shinyanga ni moja ya mikoa kame kutokana na hali hiyo upatikanaji wa vyanzo vya maji chini ya ardhi imekuwa changamoto. Hata hivyo mkoa wetu ni mnufaika wa kwanza wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria ambao kwa sasa unahudumia mikoa ya Mwanza (Kwimba na Misungwi), Shinyanga, Tabora (Igunga, Tabora na Nzega) na Mji wa Shelui Mkoa wa Singida”,ameeleza Mhandisi Payovela.
 
Amefafanua kuwa ujenzi wa miradi ya maji kupitia Bomba kuu la Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama na Shinyanga (KASHWASA), umeendelea ambapo hadi sasa jumla ya vijiji 89 vinapata maji na vijiji 50 ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji kupitia bomba hilo upo katika hatua za utekelezaji na kwamba uunganishaji wa maji ya KASHWASA umeendelea kufanyika kwa vijiji vilivyo ndani ya umbali wa km 12 kutoka bomba kuu la KASHWASA.
 
“Kwa vijiji vilivyo mbali zaidi na mtandao wa KASHWASA, tumeendelea kufanya utafiti wa maji chini ya ardhi na uchimbaji wa visima virefu hivyo mtambo huu wa kisasa ulionunuliwa kwa fedha za UVIKO-19 wenye uwezo wa kuchimba kisima hadi mita 300 utasaidia sana katika kufanikisha uchimbaji wa visima virefu kupitia RUWASA”,ameongeza.
 
Katika hatua nyingine amesema kupitia fedha za UVIKO – 19 , Mkoa wa Shinyanga ulitekeleza miradi ya maji,mradi mmoja kila Jimbo isipokuwa jimbo la Solwa imejengwa miradi miwili.
 
“Jumla ya fedha kiasi cha shilingi 3,061,459,641.73 zimetumika kutekeleza miradi 7. Miradi yote imekamilika na wananchi 26,902 wanapata huduma ya maji safi na salama”, amesema Mhandisi Payovela.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza leo Jumatatu Machi 27,2023 wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga. Kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza leo Jumatatu Machi 27,2023 wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa KASHWASA, John Zengo akifuatiwa na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, kulia ni Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola
Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela akisoma taarifa kuhusu Mtambo wa Kisasa wa kuchimbia visima virefu
Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela akisoma taarifa kuhusu Mtambo wa Kisasa wa kuchimbia visima virefu
Muonekano wa sehemu ya Mtambo wa Kisasa  wa kuchimba visima virefu vya maji 
Muonekano wa sehemu ya Mtambo wa Kisasa wa kuchimba visima virefu vya maji 
Muonekano wa sehemu ya Mtambo wa Kisasa wa kuchimba visima virefu vya maji 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (aliyevaa suti nyeusi) akikata utepe wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa KASHWASA, John Zengo akifuatiwa na Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiendesha Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.
Mtaalamu wa Mitambo kutoka RUWASA, Hamis Simwita akionesh namna ya kuongoza Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akijaribishia kuongoza Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akipiga picha na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akipiga picha na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya mapokezi ya Mtambo wa Kisasa kuchimba visima virefu vya maji Mkoani Shinyanga.
 
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Previous articleGGML, STAMICO WASAINI MKATABA WA SH BILIONI 55.2 KUCHORONGA MIAMBA
Next articleWAZAZI CCM SHINYANGA MJINI WAADHIMISHA WIKI YA WAZAZI, WAPEWA MAFUNZO YA UONGOZI, WAKEMEA AJALI ZA SIASA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here