Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ( wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Frank Nyabundege (wa kwanza kulia) wakati wa uzinduzi wa mashamba makubwa ya pamoja (block farming) uliofanyika jana Chamwino mjini Dodoma. TADB iliwapatia washiriki 812 wa programu ya kilimo biashara Building a Better Tomorrow (BBT) zana na vitendea kazi vya kilimo zenye thamani ya Shilingi milioni mia tano. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Frank Nyabundege (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana ambao ni washiriki wa programu ya kilimo biashara ‘Building a Better Tomorrow’ BBT muda mfupi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzindua programu hiyo Chamwino mjini Dodoma jana. TADB imetoa zaidi ya shilingi milioni mia tano kununua zana na vitendea kazi vya kilimo kwa ajili ya vijana 812 waliojiunga na program hiyo kwa awamu hii ya kwanza.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana ambao ni washiriki wa programu ya kilimo biashara ‘Building a Better Tomorrow’ BBT muda mfupi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzindua programu hiyo Chamwino mjini Dodoma jana. TADB imetoa zaidi ya shilingi milioni mia tano kununua zana na vitendea kazi vya kilimo kwa ajili ya vijana 812 waliojiunga na program hiyo kwa awamu hii ya kwanza.
Rais Samia alitoa pongezi hizo wakati akikagua zana na vitendea kazi vya kilimo vilivyotolewa na TADB Chinangali, Wilaya ya Chamwino kwa ajili ya uzinduzi wa mashamba makubwa ya pamoja (block farming) iliyo chini ya programu hiyo.
TADB imetoa zaidi ya shilingi milioni mia tano kununua zana na vitendea kazi vya kilimo kwa ajili ya vijana 812 waliojiunga na programu hiyo kwa awamu hii ya kwanza.