Home BUSINESS SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA MAZINGIRA WEZESHI YA WAJASIRIAMALI – MHE. KIGAHE

SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA MAZINGIRA WEZESHI YA WAJASIRIAMALI – MHE. KIGAHE

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akimkabidhi Tuzo mshindi wa kwanza aliyefanya vizuri katika kuzalisha Bidhaa za Kiasili katika hafla iliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) Machi 11,2023 katika Ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es Salaam 

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akizungumza katika hafla hiyo muda mfupi kabla ya kuanza zoezi wa utoaji wa Tuzo za Bidhaa za Viwanda Wanawake Wajasiriamali Jijini Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali na wageni walioakikwa kwenye hafla hiyo wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Kigahe alipokuwa akizungumza Katika hafla hiyo

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake kumkaribisha Mgeni rasmi.

Mwenyekiti wa TWCC Taifa Bi. Mercy Silla akizungumza alipokuwa akitoa salamu za utangulizi na kuzielezea Tuzo hizo zinazotolewa na Taasisi hiyo Kila mwaka.

Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma hamza akizungumza alipokuwa akizielezea Tuzo hizo zinazotolewa na Taasisi hiyo kila mwaka.

Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania Fatma Kange (kushoto) akimkabidhi tuzo na Cheti moja ya mshindi katika hafla hiyo

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe mwenye (suti) akicheza muziki pamoja na viongozi na wanachama mbalimbali wa TWCC katika hafla hiyo.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesema kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Wajasiriamali kupata fursa ya kuuza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Kigahe ameyasema hayo Machi 11, 2023 katika hafla ya utoaji tuzo za Wanawake wanaozalisha bidhaa za Viwandani  zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara  Wanawake Tanzania (TWCC) iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwemo TWCC imekuwa ikitambua bidhaa zinazo zalishwa  na Wajasiriamali hapa nchini na kwamba kwa kupitia majukwaa yao kumekuwa na fursa  nyingi zinazolenga kuwasaidia Wajasiriamali hao kufikisha bidhaa zao kwenye masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Aidha ameipongeza TWCC kwa jitihada kubwa wanazofanya katika kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuwawezesha na kuwainua Wanawake wafanyabiashara kote nchini.

“Ni wazi kuwa Mwanamke akiwezeshwa katika Biashara uchumi wake utaimarika na kumili kipato chake ataweza kuisaidia familia yake na kukuza uchumi wa familia na Taifa kwa ujumla” amesema Mhe. Kigahe 

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa TWCC Taifa Bi.Mercy Silla amesema kuwa Tuzo hizo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo kila mwaka TWCC inasherehekea siku hiyo kwa kuandaa maonesho ya Wajasiriamali kuonesha bidhaa zao wanazozalisha na kuhitimisha kwa hafla kubwa ya utoaji tuzo kwa Wajasiriamali wao.

Sherehe hizo za utoaji tuzo kwa Wajasiriamali ziliudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Taasisi za Umma, pamoja na Sekta Binafsi, ambapo jumla ya tuzo 70 zilitolewa.

Previous articleDC ILALA AZINDUA MSIMU WA GS1 BARCODES DAY 2023
Next articleRAIS MHE. SAMIA AMUAPISHA NAIBU KATIBU MKUU, OFISI YA RAIS TAMISEMI – IKULU CHAMWINO DODOMA 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here