NA: TIMA SULTANI
NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ( MWANA FA) ambaye ni mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mashindano ya Ramadhani Cup 2023 amewapongeza Silent Ocean kwa kuandaa mashindano hayo makubwa yenye lengo la kuibua vipaji vya wachezaji wasoka.
Naibu Waziri ameyazungumza hayo kwenye uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika usiku wa machi 27 kwenye Uwanja wa JMK Park, Jijini Dar es Salaam
Mchezo wa kwanza wa mashindano hayo ulimalizika kwa Silent Ocean FC kushinda bao 1-0 dhidi ya Discount FC ambao umechezwa saa 5:00 usiku.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Naibu Waziri, Hamis Mwinjuma amewashukuru waandaaji wa mashindano hayo Silent Ocean. kwakumpa nafasi yakuwa mgeni rasmi aliwahi kuhudhuria kipindi chanyuma lakini anaona kipindi hiki yamekuwa tofauti sana
Amesema kubwa kabisa lililomfurahisha nikufungua kwa mashindano hayo wakati timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inaingia uwanjani kuvaana na Uganda.
Naibu waziri huyo amesisitiza kuwa wao kama wapenzi wampira miongoni mwa jambo ambalo wanaweza kulifanya nikuwa wachezaji waku12 nakuwasapoti Stars katika kipindi chote.
“Mh Rais Samia Suluhu Hassan amenunu Tiketi 7000 huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akinunua tiketi 2000 hizo zote nijuhudi zakuhakikisha watu wanaend uwanjani bure hakuna anayetakiwa kukosa.
“Silent Ocean leo wameongeza tiketi 3000 na K4S Security wameongeza tiketi 1000 jumla 4000 hivyo amewataka na Yanga kuongeza tiketi 500 kati ya zile 1500 ambazo waliongeza mwanzo n Rais wa klabu hiyo ameongeza 500 ,” amesema
Aidha amekiri kuwa nafuraha kwa kupewa heshima hiyo kubwa kwenye ramadhani Cup 2023 anaamini kwa walivyojipanga inakwenda kuwa yakipekeee na alivipongeza vilabu vyote ambavyo vimejitokeza kushiriki mashindano hayo.
Naye Mtendaji Mkuu wa Silent Ocean, Mohamed Sokola, amesema kwaniaba yakampuni yao wanashukuru timu zote zilizojitokeza kwenye mashindano hayo.
“Kabla yakuanza mashindano kulikuwa nachangamoto nyingi tunaomba radhi lengo lilikuwa nikuyafanya yawe bora zaidi tunaamini mashindano haya yatakuwa mazuri kwani yanashuhurikiwa nawatu wa mpira ambao ni Chama Cha Soka Cha Mpira wa Miguu Dar es Salaam ( DRFA) ,” amesema Mohamed Soloka.