Home LOCAL MILIONI 293 ZALETA NEEMA YA MAJI KATA YA NZERA GEITA.

MILIONI 293 ZALETA NEEMA YA MAJI KATA YA NZERA GEITA.

Wakazi wa Vijiji vya Nzera na Bugando kata ya Nzera Halmashauri ya wilaya ya Geita wameipongeza serikali kwa kumaliza kero ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yao iliyodumu kwa mda mrefu.

Wakizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa maji uliopo katika kijiji cha Nzera wananchi hao wamesema tangu huru katika vijiji hivyo walikuwa hawana mradi wa maji safi na salama.

Wamesema walikuwa wanahangaika kufata maji umbali mrefu wakiamka usiku wa manane hivyo wanaipongeza serikali kuwapelekea mradi huo wa maji kwani kwa sasa huduma ya maji wanaipata kwa urahisi zaidi katika maeneo yao.

Meneja wa RUWASA wilaya ya Geita Mhandisi Sande Batakanwa wakati aakisoma taarifa mbele ya Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia mia na tayari wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama katika maeneo yao.

Amesema mradi huo utahudumia wananchi 10,448 katika vijiji viwili vya Nzera na Bugando ambapo unahusisha uchimbaji wa kisima kirefu chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 3600 kwa saa na vituo 10 vya kuchotea maji ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 100000.

Mhandisi Sande amesema mradi huo umegharimu Milioni 293.05 ambazo ni pesa dhidi ya UVIKO-19 amesema mradi huo utasaidia kupunguza mda mrefu wa kufata maji mbali pamoja na magojwa ya kuhara, homa ya matumbo yaliyokuwa yanasabaishwa na matumizi ya maji yasioyo safi na salama.

Meneja wa RUWASA mkoa wa Geita Mhandisi Jabiri Kayilla amesema mradi huo umetekelezwa kwa fedha za mpango wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 ambapo Mkoa wa Geita ulipokea bilioni 2.4 kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi ya maji katika mkoa wa Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ameipongeza RUWASA wilaya ya Geita kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maji na amewataka wananchi wa nzera na Bugando kulinda miradi ya maji pamoja na kuvuta maji majumbani kwao ili kumaliza kero ya maji.

Mbunge wa Jimbo la Geita vijijini Dkt. Joseph Msukuma amewapongeza RUWASA mkoa wa Geita hasa wilaya ya Geita kwa utekelezaji bora wa miradi ya maji ndani ya Jimbo la Geita vijijini kwani miradi mingi ya maji inatekelezwa vizuri.

Dkt. Msukuma amesema kwa sasa wananchi wanafurahia huduma hiyo ya maji safi salama amewataka wakazi wa vijiji hivyo wavute maji majumbani kwao kwani serikali imewasogezea maji kwenye maeneo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here