Home LOCAL MIKAKATI YA KUPAMBANA NA KIFUA KIKUU YAJADILIWA.

MIKAKATI YA KUPAMBANA NA KIFUA KIKUU YAJADILIWA.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Uratibu wa shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Chrispin Musiba akiongoza kikao cha Wakurugenzi  wa Wizara kwenye Mikakati ya Uwajibikaji wa Kisekta  katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu  kilichofanyika  Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi  wa Wizara kwenye Mikakati ya Uwajibikaji wa Kisekta  katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu wakifuatilia kikao  hicho.

Mshauri Mwelekezi Dkt. Oscar Mukasa akiwasilisha mada katika kikao cha Wakurugenzi  wa Wizara kwenye Mikakati ya Uwajibikaji wa Kisekta  katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu  kilichofanyika  Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

Mratibu wa Uraghibishi na Mawasiliano Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu  na Ukoma kutoka Wizara ya Afya Bw. Julius Mtemanji (kulia) akifafanua jambo katika kikako hicho.

Mratibu wa Masuala ya ugonjwa wa Kifua Kikuu  na UKIMWI  kutoka Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Adela Mpina akieleza jambo katika kikao hicho.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Wakurugenzi  wa Wizara kwenye Mikakati ya Uwajibikaji wa Kisekta  katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu  wamekutana Jijini Dodoma kujadili masuala mbalimbali kuhusiana na ugonjwa wa Kifua Kikuu na namna bora ya kuboresha  huduma ya afya.

Kikao hicho kilifanyika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu kikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Uratibu wa shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Chrispin Musiba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here