Home BUSINESS MIAKA MIWILI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA UMELETA MAFANIKIO CHANYA WCF

MIAKA MIWILI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA UMELETA MAFANIKIO CHANYA WCF

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma (Katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile (kulia) na Mkurugenzi wa Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha kuwaelimisha wanachama wa TEF kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi .


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile.
Washiriki wakipatiwa mafunzo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter.
Mkurugenzi wa Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria WCF, Abraham Siyovelwa.
Mkuu wa Hadhari WCF, James Tenga
Baadhi ya Wahariri wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa.
Baadhi ya Wahariri wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano WCF Laura Kunenge akijibu baadhi ya hoja kutoka kwa washiriki.
Picha ya pamoja.

NA: K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, BAGAMOYO

KUMEKUWEPO na maendeleo chanya katika utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) kutokana na mabadiliko ya Kisera ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF,  Dkt. John Mduma wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kilichofanyika wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Machi 20, 2023.

Alisema katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumeshuhudiwa kupunguzwa kwa tozo mbalimbali.

“Wafanyabiasha kwa maana ya sekta binafsi walipaswa kuchangia asilimia 1% ya mshahara wa mfanyakazi kila mwezi na ilipunguzwa hadi kufikia asilimia 0.5%,  kwa wafanyabiashara hii ni nafuu kubwa katika muktadha wa utekelezaji wa Blue Print wa kuweka mazingir ya uwekezaji na ufanyaji biashara Tanzania kuwa mazuri.” Alifafanua.

Jambo lingine ni kupunguzwa kwa kiwango cha riba cha asilimia 10% hadi asilimia 2% kwa mwezi kwa wanaochelewesha kuwasilisha michango ya kila mwezi.

“Mzigo huu ulikuwa ni mkubwa sana na ulikuwa unatishia wale ambao walipaswa kujisajili kwenye Mfuko kuja kujsiajili, kupunguzwa kwa riba hii kumewavutia wafanyabiashara na hivyo kuongeza idadi ya wanachama kujisajili na Mfuko.” Alisema Dkt. Mduma.

Mafanikio mengine aliyataja kuwa ni pamoja na kuhakikisha kipato cha Mfanyakazi wa Kima cha chini anayeugua, kuumia kutokana na kazi na asilimia anazopata kutokana na ulemavu au ugonjwa , Serikali ya awamu ya sita imeweka kima cha chini cha fao kuwa shilingi 270,000/=.

“Hili ni jambo ambalo serikali imefanya makusudi ili kuhakikisha kwamba wote wanaopata madhila wakiwa kazini hawadumbukii kwenye lindi la umasikini na wale wategemezi wao wananyanyuliwa zaidi.” Alibainisha.

Aidha Dkt. Mduma alisema jambo lingine ambalo limeongeza ufanisi kwenye utoaji huduma wa Mfuko ni matumizi ya Tehama kwa zaidi ya asilimia 85.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deogadus Balile amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
maelekezo yake ya kutaka taasisi za Umma kuwapunguzia mzigo wananchi na kutoLea mfano WCF, kwa kutekeleza maelekezo hayo kwa kupunguza viwango vya uchangiaji.

Aidha Mwenyekiti huyo pia alipongeza mageuzi makubwa ya utoaji huduma yaliyofanywa na WCF katika miaka ya hivi karibuni ambapo kwa sehemu kubwa huduma zimehama kutoka matumizi ya karatasi na kuwa ya Kidijitali.

“Kwaweli  huko nyuma huduma zilikuwa kwenye makaratasi,
sisi wengine tunatokea upande wa waajiri siku hizi ushindwe kujikadiria wewe mwenyewe, ukitaka kufanya malipo unaingiza takwimu halafu inakueleza unapaswa kulipa kiasi gani na unapatiwa Control number ili kufanya malipo.” Alisema.

Kuhusu mafunzo yaliyotolewa kwenye kikao hicho, Wahariri wamepata fursa ya kuelewa Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi iliyowasilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Sheria WCF, Abraham Siyovelwa.

Pia walijifunza taratibu za kuwasilisha madai ya Fidia, ambapo Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter aliwapitisha hatua kwa hatua kuhusu namna Mwajiri au mfanyakazi anavyoweza kuwasilisha madai.

Aidha Mkurugenzi wa Tathmini Dkt. Abdulsalaam Omar, aliwaeleza washiriki hatua mbalimbali za kufanya tathmini kwa mfanyakazi aliyeumia ama kuugua kutokana na kazi ili aweze kupatiwa Fidia stahiki.

Washiriki pia walipata fursa ya kuelezwa ustahimivu na uendelevu wa Mfuko katika kutoa huduma za ulipaji wa Mafao ya Fidia ambapo Mkuu wa Kitengo cha Hadhari, James Tenga alibainisha kuwa  Mfuko uko madhubuti na utaendeleas kutoa huduma za ulipaji wa Mafao ya fidia stahiki na kwa wakati

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here