KIKOSI cha KMC FC kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa Ligi kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Geita ambapo utacheza Aprili 11 badala ya 17 kama ilivyokuwa imepangwa awali na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB.
Kwa mujibu wa barua ya TPLB iliyotumwa Machi 20 mwaka huu ilieleza kuwa mchezo huo umefanyiwa mabadiliko ya tarehe kutokana na kuwepo kwa ratiba ya robo fainali ya michuano ya kombe la Azam Sport Federation na kwamba wachezaji wanaendelea kujifua kwa ratiba hiyo.
KMC FC itakuwa nyumbani katika mchezo huo ambapo Kocha Mkuu Thierry Hitimana anaendelea na programu za kukinoa kikosi hicho kwa ratiba mpya lengo ikiwa ni kupambana ili Timu iwezekupata matokeo mazuri licha ya kwamba utakuwa naushindani mkubwa.
” Tangu Timu ilipoingia kambini Machi 19 mwaka huu imekuwa na morali kubwa pamoja na kujituma zaidi mazoezini jambo ambalo linaleta hamasa na hari ya ushindani kwenye mchezo huo, mashabiki zetu wasiwe na wasiwasi kwasababu wachezaji wetu wapo kwenye hali nzuri.
Hata hivyo ” Hivi sasa Ligi inakwenda ukingoni kutokana na kwamba KMC FC tumebakiza michezo mitano ambapo tunahitaji kupata matokeo mazuri ili kujiimarisha zaidi kwenye msimamo tofauti na hivi sasa ambapo tupo katika nafasi ya 12 ambayo sio nzuri ukilinganisha na Timu nyingine.
KMC FC ipo nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara ikiwa imecheza jumla ya michezo 25 huku ikibakiza mitano ambayo ni dhidi ya Geita Gold, Dodoma Jiji, Singida Bigi stars, Tanzania Prisons pamoja na Mbeya City.
Imetolewa leo Machi 22
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano KMC FC