Home LOCAL KATIBU MKUU DKT. YONAZI APOKELEWA RASMI OFISI YA WAZIRI MKUU AOMBA USHIRIKIANO

KATIBU MKUU DKT. YONAZI APOKELEWA RASMI OFISI YA WAZIRI MKUU AOMBA USHIRIKIANO

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo Februari 28, 2023Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Stella Mwaiswaga akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo wakati wa haflaya kumpokea kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi.

Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya mapokezi mara baada ya kuwasili rasmi Ofisini hapo Jijini Dodoma tarehe 28 Februari, 2023. Baadhi ya Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya mapokezi.

NA: MWANDISHI WETU- Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi  amepokelewa rasmi  katika Ofisi ya Waziri Mkuu  hii leo Februari 28, 2023 Jijini Dodoma na kutoa wito kwa Menejimenti na watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu kwa lengo la kuleta ufanisi.

Dkt. Yonazi amewasihi watumishi hao kufanya kazi kwa juhudi, upendo na Amani ili kuwatumikia wananchi na kuifaya Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea na jukumu lake kubwa la kuratibu shughuli za Serikali kwa matokeo chanya.

Katika hafla hiyo ya mapokezi amewasihi watumishi kuwa wamoja na kufanya kazi kwa weledi zaidi huku akiwashukuru kwa mapokezi mazuri.

“Nimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Sulluhu Hassan kwa kuniteua kuitumikia nafasi hii, ikumbukwe  kuwa tuna jukumu kubwa la kuwatumikia wananchi hivyo tufanye  kazi kwa juhudi huku tukidumisha ushirikiano,” Alieleza Dkt. Yonazi.

Previous articleWAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA KIPIMO CHA BIDOO
Next articleSENYAMULE AHIMIZI BALOZI KUJENGA DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here