Home LOCAL KATIBU MKUU CCM AVUNJA UKIMYA WANAOPOTOSHA KUHUSU KUKOPA

KATIBU MKUU CCM AVUNJA UKIMYA WANAOPOTOSHA KUHUSU KUKOPA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi ya Hospitali ya Kiomboi Daktari Abel Mafuru ya vifaa tiba vya kisasa katika wodi za dharura na la wagonjwa mahututi Wilayani Iramba mkoa wa Singida.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Iramba Ndugu Mwigulu Mchemba (kushoto) wakati wa kikao cha wanachama wa CCM wa shina namba 6, Tawi la Ulemo Kata ya Ulemo wilayani Uramba, katikati ni Mwenyekiti wa shina hilo Ndugu Evangelina Petro Samuel.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema akihutubia wakazi wa shina namba 6, Ulemo wilayani Iramba mkoa wa Singida.

Wanachama wa CCM wa shina namba 6, Tawi la Ulemo Kata ya Ulemo wilayani Uramba wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo.
*Asema hakuna nchi isiyokopa duniani, hata Marekani inakopa*Aweka wazi Tanzania ina mzigo mdogo wa madeni Afrika Mashariki

Na: Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amewaomba wananchi kutowasikiliza watu ambao wamekuwa wakizusha maneno ya uongo wa kwamba Tanzania inakopa sana , ukweli uliopo nchi yetu ndio ambayo haina mzigo mkubwa wa mikopo kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Chongolo ametoa kauli hiyo leo mkoani Singida wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ulemo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi sambamba na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025.

Chongolo ameyazungumza hayo leo Machi 01, 2023 wakati wa kikao cha shina namba 6 Katika kata ya Ulemo, Wilaya ya Iramba ikiwa ni Siku ya Tatu ya Ziara yake mkoani Singida.

“Wapo jamaa ambao wanapiga kelele wanasema tunakopa sana , nataka niwaambie katika nchi za Afrika Mashariki nchini ambayo haina mzigo wa mikopo kuliko nchi nyingine zote ni Tanzania.Na kwanini hicho wanachopigia kelele kukopa?

“Hakuna nchi duniani ambayo haikopi, nitawapa mfano hivi karibuni huko duniani Marekani ilikopa kwa China, wote si mnajua Marekani ndio dunia nyingine , watu wote si mnajua ukisema Marekani ndio kila kitu lakini nendeni mkapekue na mjiridhishe na ninachosema.

“Mimi ni kiongozi mkuu wa Chama siwezi danganya , nimetaja kwa jina kwasababu ni ukweli sio tu habari inatoka kwangu imeandikwa na mtaipata hata kwenye mitandao .Marekani ilikwenda kukopa kwa China na niambieni hapa kuna hajui kukopa , kuna mtu amewahi kuonekana wa hovyo kwa kukopa ?

“Sisi ambao tumekuwa watumishi ulizeni mtumishi ambaye hajakopa anyooshe mkono mimi sijakopa. Lakini ninachosema ni nini ? Mtu yoyote ambaye anataka usiendelee anakufunga na kukutengenezea mazingira yaw ewe kujifunga kama kisiwa ili watu wako wabakie vile vile,” amesema Chongolo

Ameongeza kuwa hata ukiangalia historia ya nchi hii mwaka 1961 wakati tunakabidhiwa kwenye kihenge kulikuwa hakuna hata senti moja, Wakoloni walikuwa wamesomba kila kitu lakini Mwalimu Nyerere baada ya kukabidhiwa nchi ndani ya miezi miwili alianza kukopa.

Amesema alikopa ili kujenga nchi inayojitegemea na hivyo hivyo hata ukiwa mtumishi au mfanyabiashara unakopa ili kuboresha na kuimarisha uchumi wako , hukopi ili kwenda kuoa na hakuna anayekwenda kukopa kwa ajili ya kwenda kuoa.

“Tunakopa ili kufanya maendeleo kwa wananchi na sisi kurudisha taratibu kwa kile tunachokipata, ndio historia ya nchi inayojitambua. Nchi zote zinakopa ,sisi leo tunazungumzia umeme , hivi umeme usingekuwepo Ilemo ungeenda kufuata umeme wapi?Singida au Kiomboi?Lakini leo kwa fedha zetu tunao umeme.

“Kama mtu halipi deni unamkopesha? Ukiona unakopesheka ni kwasababu muaminifu na unalipa deni, sasa msikae na maneno ya watu ambao hawaitakii mema nchi yetu. Nchi yetu inakopa na nchi nyingine zote zinazotuzunguka zinakopa.

“Nchi zote nyingine zote duniani zinakopa zinapokuwa na masuala mahususi ambayo wanadhani kwa kupata fedha na kuyatekeleza yana tija kwa wananchi .Leo hii barabara ya Singida tulikopa zaidi ya miaka 30 iliyopita barabara ilejengwa deni tulimaliza kulipa.

“Hii barabara imeondoka? Wote ni mashahidi mlima nyoka na Sekenke mnakumbula ilikuaje, leo hata ukiwa na bajaji unapanda .Tungekaa kienyeji leo tusingekuwa tunapendeza , unaweza kwenda kahama kuuza ndizi na ukarudi . Sababu Serikali inapanga na kutekeleza mipango yake na hiyo ndio kazi ya Serikali .

“Acheni kudanganywa, achene kusikiliza kila mtu anayesema chochote wapo waliopewa kazi ya kutengeneza uongo na wapo waliopewa kazi ya kutekeleza. Tusidanganyike kazi ya kuongoza nchi ni kazi kubwa, ni kazi inayohitaji mipango ya muda mrefu,”amesema Chongolo.

Ameongeza kwamba ukipanga vizuri mambo yako yanaenda vizuri, ndio maana mara nyingine mnaona Mbunge wenu wanamtupia maneno mengi lakini ameshakomaa na huo ndio uongozi.

“Anabeba matusi kwasababu ya niaba yenu na kiongozi mzuri ni yule ambaye hatetereki kwa maneno,Chama Cha Mapinduzi kingekuwa kinasikiliza maneno sasa tungekuwa tumelala wote hoi.

“Tunawaza hivi jamaa wametusema kiasi gani lakini tusiposemwa na sisi hatutafanya vizuri na waacheni wasema maana ndio kazi wanayoijua.Uongo unaenda kama jeti , ukweli unatembea kama lori.

Previous articleTMDA YAPIGA MSASA KWA WATOA HUDUMA MKOA WA IRINGA
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 2,2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here