Home LOCAL WIZARA YA AFYA YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE DODOMA

WIZARA YA AFYA YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE DODOMA

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya afya na masuala ya UKIMWI wakiongozwa na Mwanyekiti wa kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo wamekutana na viongozi kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake wakiongozwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Seif Shekalaghe katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.

Katika kikao hicho Wizara imewapitisha wajumbe wa kamati hiyo juu ya shughuli na majukumu ya kila Idara na vitengo vilivyo chini ya Wizara afya pamoja na kuelezea mikakati mbalimbali ya Wizara katika kuimarisha ubora wa huduma ikiwemo huduma za UKIMWI nchini.

#MtuNiAfya
#JaliAfyaYako

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here