Halmashauri ya Jiji la Tanga imefanikiwa kuvuka lengo la uandikishaji wa darasa la awali kwa mwaka huu wa 2023 kwa kuandikisha wanafunzi 6833 sawa na asilimia 106.Hayo yamesemwa na Ofisa Elimu wa Awali na Msingi Kassim Kaoneka wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika ofisini kwake kutaka kujua hali ya uandikishaji katika Jiji hilo umefikia asilimia ngapi ukilinganisha na mwaka jana.
Kaoneka alisema kuwa Kwa mwaka huu walitarajia kuandikisha wanafunzi wa awali 6417 lakini wamevuka lengo nakufikia 6833 ambapo kati yao wavulana ni 3559 huku wasichana waliondikishwa ni 3274 huku mwaka jana walioandikishwa walikuwa walikuwa 7249.
“Licha ya kuvuka lengo Kwa mwaka huu lakini pia bado milango ya uandikishaji ipo wazi hadi ifikapo march 30 mwaka huu” Alieleza Ofisa Elimu huyo.
Ofisa Elimu huyo alieleza kuwa muitikio huo wa uandikishaji unatokana na uhamasishaji uliofanywa kwa Wazazi ,Walezi na jamii katika maeneo mbalimbali katika Jiji hilo.
Kwa upande wao Wazazi walisema kilichowavutia mwaka huu kuwaandikisha watoto wao wenye umri wa kwenda shule ni kutokana na mazingira mazuri yaliopo katika shule mbalimbali za Jijini hapa pamoja na uboreshaji wa miundombinu uliofanywa hasa katika madarasa ya awali.
Mwanahamisi jumaa Mkazi wa kasera alieleza kuwa yeye anatambua umuhimu wa elimu ndio maana mtoto wake alipofikisha umri wa kwenda shule akaona amuandikishe ili aweze kupata haki yake ya msingi.
Shewali Hoza Mkazi wa mikanjuni ambaye ni baba wa watoto wawili mapacha yeye alisema kuwa kuwa yeye hakupata fursa ya kusomeshwa kulingana na changamoto za hapa na pale hivo aliahidi yeye na mkewe watoto wao watakapofikisha umri wa kwenda shule atawapeleka ili waweze kupata msingi mzuri wa elimu kuanzia wakiwa wadogo.
Kupitia Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto( PJT- MMMAM) 2021/22- 2025/26 inaonyesha Tanzia ni nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki katika elimu ya awali kuifanya kuwa lazima kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ili kujumuisha elimu ya awali katika elimu ya msingi Kwa kuzitaka shule zote za msingi kuwa na darasa elimu ya awali Kwa watoto wa chini ya miaka mitano.
Vile vile ,Mtaala wa Elimu wa elimu ya awali unaosaidia ujifunzaji kupitia Michezo na muongozo wa Serikali wa mwaka 2016 wa elimu bila malipo hujumuisha elimu ya awali, nakuongeza kuwa uandikishwaji wa elimu ya awali ni kiashiria muhimu kilichoingizwa katika mpango wa kitaifa wa maendeleo ya miaka mitano 2016/17-2020/21
Hata hivyo kutokana na kuongezeka Kwa idadi ya watoto walioandikishwa katika shule za awali ,idadi ya walimu bado haitoshi .
Wadau wanaotekeleza program za MMMAM nchini kama vile Children inCrossfire na Shirik a lakuhidumia watoto Duniani (UNICEF ) wameweza kutekelezaprogram ya mafunzo Kwa walimu wa shule za awali waliokazini ili kutoaelimu bora Kwa watoto katika mazingira yenye watoto wengi wenye uhitaji,mafunzo yao yamezingatia Sera ya Elimu na Mafunzo pamoja na mitaala ya Elimu ya Awali iliyotolewa na Taasisi ya elimu Tanzania.
CREDIT: MICHUZI BLOG