Home SPORTS FREDERICO WA SINGIDA BIG STARS AONGEZEWA MUDA WA UANGALIZI

FREDERICO WA SINGIDA BIG STARS AONGEZEWA MUDA WA UANGALIZI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

MCHEZAJI wa Singida Big Stars Dario Frederico, amemaliza likizo yake ya mwezi mmoja na ripoti ya daktari inaonesha amepona kwa zaidi ya 90%.

Hata hivyo, klabu kupitia kwa ushauri wa kitaalamu wa daktari imemuongezea muda Dario Jr ili aweze kuwa timamu kwa 100% apate na muda wa kutosha wa kupumzika.

Kutokana na maamuzi haya, mchezaji huyo raia wa Brazil ataungana na kikosi rasmi wakati wa maandalizi ya ligi kuu msimu ujao wa 2023/24.

Wadau na mashabiki wa Singida Big Stars watarajie kumuona Dario akiwa kwenye kiwango bora zaidi atakapoungana na timu kwenye kambi yetu ya Pre-season nchini Tunisia.

Taarifa hiyo imetolewa hivi karibuni na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hussein Masanza.