Home Uncategorized DKT. MOLLEL ATOA WITO KWA WANAKAGERA KUFUATA MAELEKEZO YA WATAALAMU.

DKT. MOLLEL ATOA WITO KWA WANAKAGERA KUFUATA MAELEKEZO YA WATAALAMU.

Na: WAF – KAGERA.

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel kwa niaba ya Waziri wa Afya amewaasa wananchi wa Mkoa wa Kagera kufuata maelekezo ya Wataalamu wa afya katika maeneo yao ili kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya mlipuko.

Dkt. Mollel ametoa wito huo leo Machi 18, 2023 wakati akiongea na vyombo vya habari baada ya kufanya kikao na Wataalamu wa afya katika Mkoa huo ili kuona namna bora ya kupambana dhidi ya mlipuko ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

“Tuendelee kuwaasa wananchi maelekezo yote ambayo Wataalamu wa afya wanayatoa mfano mambo ya kuzikana, hata kama mgonjwa hajaonesha dalili zinazofanana kama swala la maziko wayazingatie kwa Wataalamu na maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya.” Amesema.

Aidha, Dkt. Mollel ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa namna walivojitoa katika kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali tangu kuibuka kwa ugonjwa usiojulikana Machi 16, 2023 Mkoani hapo.

Sambamba na hilo amewapongeza Watumishi wa afya katika ngazi zote, kuanzia ngazi ya Mkoa mpaka ngazi ya zahanati kwa namna bora wanavoendelea kupambana katika utoaji huduma jambo ndio maana bali ya afya inaendelea kuimarika.

Pia, amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa pesa, vifaa, dawa na rasilimali watu ili kuhakikisha hali ya afya katika Mkoa wa Kagera inaimarika na utoaji huduma unakuwa bora.

Mwisho

Previous articleDIWANI WA KIPAWA AMEWASHAURI WAZAZI KUCHANGIA CHAKULA CHA WANAFUNZI SHULENI
Next articleSIMBA SC YAOGELEA MINOTI YA MAMA, YAIFUMUA HOROYA FC 7-0 KWA MKAPA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here