Home LOCAL DIWANI WA KIPAWA AMEWASHAURI WAZAZI KUCHANGIA CHAKULA CHA WANAFUNZI SHULENI

DIWANI WA KIPAWA AMEWASHAURI WAZAZI KUCHANGIA CHAKULA CHA WANAFUNZI SHULENI

Na: Heri Shaaban (Ilala )

Diwani wa Kata ya Kipawa Idani kwezi, amewashauri Wazazi wa Wanafunzi shule Kata Kipawa kuchangia CHAKULA kwa ajili ya Wanafunzi shuleni waweze kufanya vizuri kitaaluma.

Diwani wa kipawa Idani kwezi, alitoa ushauri huo Leo katika kikao cha wazazi shule ya Sekondari Majani ya Chai Wilayani Ilala akiwataka wazazi wa kipawa kutoa ushirikiano kwa walimu kuchangia CHAKULA Ili wanafunzi waweze kula.

“Nawahimiza Wazazi kuinua taaluma shuleni wanafunzi wawe na nidhamu watoe ushirikiano baina ya wazazi , Walimu na Wanafunzi Ili waweze kufanya Vizuri darasani kitaaluma “ alisema Aidani 

Aidha Diwani Aidani Kwezi aliwahimiza wazazi kushiriki kikamilifu katika utekekezaji wa sera ya chakula shuleni kama Serikali ilivyotoa mwongozo .

Diwani Aidan Kwezi alitumia nafasi hiyo katika kikao cha shule na wazazi kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa pesa nyingi katika sekta ya Elimu kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ambaopo wameshapokea milioni 120 kwa ajili ya kujenga vyumba sita vya Madarasa na madawati 400 wanajivunia Kipawa Serikali ya awamu ya sita imefanya mambo makubwa.

Pia aliwapongeza Walimu wa shule ya Sekondari Majani ya Chai ,Walimu na Wanafunzi kuendelea kujitoa kwa nguvu zote na kuhakikisha ufaulu unaongezeka na Wanafunzi wanapata alama nzuri .

Mwisho.

Heri Shaaban
Habari 0714 872471
0755 872471

Previous articleSHABIKI WA SIMBA : HOROYA FC WATUSAMEHE TU, LEO HAWATOKI KWA MPAKA
Next articleDKT. MOLLEL ATOA WITO KWA WANAKAGERA KUFUATA MAELEKEZO YA WATAALAMU.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here