Home LOCAL DIWANI AIDAN KWEZI WA KIPAWA ANATOSHA 2025

DIWANI AIDAN KWEZI WA KIPAWA ANATOSHA 2025

Diwani wa Kata ya Kipawa Aidan Kwezi akizungumza na Watoto wa Makundi maalum Kata ya Kipawa (Picha na Heri Shaaban )

Diwani wa Kipawa Aidan Kwezi akigawa chakula Kwa Watoto wa Mazingira magumu katika siku yake ya kuzaliwa Machi 02/2023 (Picha na Heri Shaaban ).

Diwani wa Kata ya Kipawa Aidan Kwezi akiwa na Viongozi wa Kata ya Kipawa wakiomba Dua ya ufunguzi katika halfa ya siku yake ya kuzaliwa Machi 02/2023 (Picha na Heri Shaaban )

Na: Heri Shaaban (Ilala)

Diwani wa Kata ya Kipawa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Aidan Kwezi, anatosha kuendelea nafasi yake ya Udiwani wa Kipawa kwa utekekezaji Ilani kwa vitendo ndani ya Kata ya Kipawa .

Hayo yalisemwa na Katibu wa Kata ya Kipawa Jafari Napinda wakati wa siku ya kuzaliwa Diwani Aidan Kwezi, katika chakula cha jioni na Watoto yatima kituo Cha Zilihouse of Child Care.

“Diwani Aidan Kwezi anatosha 2025 kuendelea na udiwani wake Kipawa ni mtu anayejituma kwa Wananchi wake katika shughuli za kijamii na pia anatekeleza Ilani wa vitendo pamoja na kumsaidia makundi maalum “ alisema Jafari.

Katibu Jafari alisema Diwani Aidani Kwezi anashiriki matukio mbalimbali ya Kijamii ikiwemo kufanya ziara katika vituo mbali vya yatima ambapo siku yake ya kuzaliwa Leo ametumia kura chakula na Watoto wa Makundi maalum wanaolelewa Kata ya Kipawa .

Alisema kwa Diwani Aidani mpaka Sasa anatosha kuendelea kuongoza Wananchi wa Kipawa amewataka wampe Ushirikiano katika kujenga chama na Serikali .

Mwenyekiti wa CCM kata ya Kata ya Kipawa Saidi Mkuwa, aliwataka Wadau na madiwani kushirikiana kulea Watoto wa kituo hicho Ili waweze kufikia malengo yake .

Mwenyekiti Saidi Mkuwa alisema ni kweli Diwani Aidan anatosha ni mtu ambaye anajitoa kwa jamii yake inayomzunguka na anajitolea vizuri na kazi za chama anashiriki vizuri Utekelezaji wa Ilani .

Mwenyekiti Saidi Mkuwa aliwataka wale wote WALIOANZA kunyemelea Kata ya Kipawa wakae pembeni Diwani Aidan kwezi anatosha .

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Umoja wanawake UWT WIlaya ya Ilala Elizabeth Kilele Mama Zoa Zoa alimpongeza Diwani Aidan kwa kuzaliwa siku ya Leo ameonyesha upendo kwa jamii yake .

Elizabeth Kilele Mama Zoazoa aliwataka wananchi wa Kipawa kumpa Ushirikiano Diwani katika kazi zake anazofanya za Utekelezaji wa Ilani katika Juhudi za kumsaidia Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan .

Diwani wa Kipawa Aidan Kwezi ,alisema changamoto za Kituo Cha Zilihouse of Child Care walizipokea hivi karibuni walivyofanya ziara Leo wamezitatua Kwa kushirikiana na UWT Kipawa na Mama Maendeleo wa Kata .

“Nimetumia siku yangu ya kuzaliwa Leo katika kituo hichi Cha Watoto wa Makundi maalum kula chakula pamoja na kuwapa pesa za Bima ya Afya Watoto wa kituo hichi Cha Zilihouse of Child Care nimefarijika Sana naomba Wadau wengine watembelee kituo hichi kuwaunga Mkono “alisema Aidan .

Diwani Aidani Kwezi aliwashukuru viongozi wa chama na Serikali pamoja na madiwani wezake wa Hal mashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kumpa Ushirikiano katika utekekezaji wa Majukumu yake .

Aliwataka Watoto wa kituo hicho wawe na nidhamu wazingatie masomo Ili waweze kufikia malengo yao Kituo Cha Zili House of Child Care kilichopo Kipawa Wilayani Ilala kilianzishwa mwaka 2021 mpaka Sasa kina Watoto Kumi na Moja wapo shule ya Msingi na Shule ya Awali .

Wakati huo huo Diwani Aidan Kwezi alisema kata ya Kipawa imepata Miradi ya Maendeleo katika utekekezaji wa Ilani ya chama aliwataka Wananchi wake kutunza Miradi hiyo na kutangaza kazi zinazofanywa na Mh,Rais Samia Suluhu Hassan .

Mwisho

Heri Shaaban
Mwandishi
0714 872471
0755 872471

Previous articleDC MAGEMBE, AJA NA MKAKATI MPYA KUDHIBITI MATUKIO YA MAUAJ WILAYA YA GEITA.
Next articleBENKI YA CRDB YATWAA TUZO YA BENKI BORA KATIKA UTOAJI HUDUMA KWA WAJASIRIAMALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here