Home LOCAL DC MPOGOLO AONGOZA KAMPENI YA USAFI ILALA

DC MPOGOLO AONGOZA KAMPENI YA USAFI ILALA

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo(katikati) akiongoza wananchi wa Wilaya ya Ilala katika Kampeni endelevu ya usafi kuanzia Uwanja Ndege mpaka Barabara ya Nyerere Leo Machi 25/2023 (kutoka kulia)Diwani wa Kipawa Aidani Kwezi na Mkurugenzi wa Kampujni ya usafi Kajenjele na Diwani wa Viti Maalum wilaya ya Ilala Magreth Cheka (Picha na Heri Shaaban)

Mkandarasi wa Usafi Kampuni ya Kajenjele akishiriki usafi kuunga mkono juhudi za Serikali za kupendezesha Dar es Salaam (Picha na Heri Shaaban)

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akiongea na Wananchi wa Wilaya ya Ilala baada kumaliza kampeni endelevu ya usafi Leo(kushoto )Diwani wa Kipawa Aidan KWEZI (picha na Heri Shaaban.

AFISA Mazingira Wilaya ya Ilala Theresa Mwakasungula akiwa na Afisa Usafishaji Halmashauri ya Jiji Methew Mayonga Barabara ya Nyerere Leo Machi 25/2023 wakati Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo alipokuwa akiongoza Kampeni ya usafi (Picha na Heri Shaban)

Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Kipawa wakishiriki Usafi barabara ya Nyerere Leo (Picha na Heri Shaaban)

Na: Heri Shaaban (Ilala)

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ameongoza Kampeni ya Usafi Wilaya ya Ilala kwa kusafisha eneo la Uwanja Ndege na Barabara ya Nyerere.

Akizundua Kampeni hiyo ya Usafi Ilala Leo Pamoja Wakandarasi wa Usafi waliojitokeza kuunga mkono Juhudi za Serikali ,Kampuni za Kajenjele ,Kampuni ya SATEK na KIMWEDE , Mkuu wa Wilaya Mpogolo alitoa agizo viwanda vya Barabara ya Nyerere na Kampuni zilizopo Barabara hiyo kupaka Rangi majengo na kupendezesha maeneo yao.

Akitoa agizo hilo leo alisema kampeni ya usafi Wilaya ya Ilala inaunga mkono agizo la Mkuu wa Mkoa la kupendezesha mji wa Dar es Salaam kuweka maeneo yote katika hali ya Usafi.

“Naagiza makampuni ya Barabara ya Nyerere na viwanda wakikishe yanapaka Rangi majengo yao kwa ajili ya kupendezesha Mji wetu Kila wakati uwe msafi “ alisema Mpogolo .

Wakati huo huo alitoa agizo kwa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam kuboresha K
Kwa kutunza Mazingira barabaraba ya Nyerere mpaka Ikulu Wilayani Ilala .

Katika hatua nyingine alisema kesho kutwa tunatarajia kupokea ugeni mzito katika nchi yetu Makamu wa Rais wa Marekani anafanya ziara ya kikazi hapa nchi hivyo tuakukikishe tunatunza mazingira kwa usafi ,ugeni Makamu wa Rais wa Marekani ni fursa kwa nchi yetu Tanzania .

Meneja Mahusiano Benki ya Kanda ya Dar Es Salaam Irene Masaki, alisema usafi iwe tabia yetu maelekezo yaliotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala wameyapokea watatekelezwa.

Diwani wa Viti Maalum Magreth Cheka alisema suala la usafi iwe endelevu Wilaya ya Ilala Wananchi tufanye Kila wakati .

Diwani wa Kipawa Idani Kwezi alisema Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ni mchapakazi Wana Ilala tushirikiane naye katika kudumisha usafi pamoja na kuleta maendeleo .

Diwani Aidani Kwezi alisema kampeni ya usafi iwe Kila siku ikifika mwisho wa mwezi kampeni inaitimishwa .

“Kata yetu ya Kipawa tupo katika Kampeni endelevu ya Kipawa ya Kijani tumejipanga kupanda miti 10000 Kwa ajili ya kusaidia serikali kutunza Mazingira Yetu “ alisema Idani .

Mwisho

Previous articleTANROADS IMEWATAKA WATUMISHI WAKE KUTENGA MUDA WA MAZOEZI
Next articleTGNP NA DIT KUJA NA SULUHISHO LA MASUALA YA JINSIA KWA NJIA YA KIDIJITALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here