Home BUSINESS DC ILALA AIPONGEZA GS1 KUWAJENGEA UWEZO WAZALISHAJI

DC ILALA AIPONGEZA GS1 KUWAJENGEA UWEZO WAZALISHAJI

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Edward Mpogolo, aanza kazi na #GS1 kwa kufungua mafunzo kwa Mradi maalum ya Kujengea uwezo wazalishaji ngazi ya Halmashauri nchini wa GS1 Tanzania katika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Mradi huu ni ili wazalishaji waweza kuuza nje kimkakati. Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Anatoglo jijini DSM Jana.

Katika Maelekezo alihamasisha Halmashauri zingine kuweza kuunga mkono mpango huo wa GS1 Tanzania wa kutoa mafunzo Ngazi za Halmashauri kwani mradi huo una malengo endelevu kwa Sekta ndogo ya Wazalishaji na Biashara
Nchini.

Katika Mkoa wa DSM Halmashauri ya Ilala ndio imekuwa ya kwanza kwa kulipia gharama za mafunzo hayo yenye tija kubwa kwa wazalishaji nchini.

Amevutia na Mkakati wa GS1 Tanzania 2023 wa “Mkakati Ibua Viwanda” na kampeni ya GS1 Beyond Barcodes iliyokuja nayo katika kumuunga mkono Mhe Raisi ya kuendekeza Private Sector nchini. Mkuu wa Wilaya ya Ilala athibitisha kuzipa shughuli za GS1 Kipaumbele kikubwa katika kujenga sekta ndogo ya Biashara.

Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Bi Fatma Kange ameshukuru kwa namna shughuli za GS1 Tanzania zinavyoendelea kuungwa mkono na Serikali na taasisi za sekta Binafsi kwa manufaa ya wananchi wote na Taifa kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here