Home LOCAL DAWASA YASHIRIKI KONGAMANO LA PILI LA KIMATAIFA LA KISAYANSI LA MAJI, WADAU...

DAWASA YASHIRIKI KONGAMANO LA PILI LA KIMATAIFA LA KISAYANSI LA MAJI, WADAU WAKUTANA KUJADILI TAFITI.

Na: Neema Mbalamwezi

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) ni moja kati ya Taasisi za Serikali pamoja na Sekta binafsi zinazoshiriki Kongamano la pili la Kisayansi la maji likiwa na lengo la kuwakutanisha wadau na wanazuoni kujadili tafiti mbalimbali za sekta ya maji.

Akizungumza wakati akifungua Kongamano hilo, Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso (Mb) ametaka Kongamano hili kuwa endelevu na kuleta majibu ya changamoto mbalimbali katika sekta ya maji.

“Kongamano hili la maji likawe sehemu ya kutuletea majibu ya changamoto juu ya sekta ya maji nchini, kupitia wataalamu mbalimbali, changamoto mbalimbali zikajibiwe.” ameeleza Mhe. Aweso

Waziri Aweso ameongeza kwa kukipongeza chuo Cha Maji kwa kazi nzuri inayoendelea kufanyika, huku akiahidi Wizara kutoa ushirikiano ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya maji Mhandisi Cyprian Luhemeja amewahakikishia wadau wa sekta ya maji kuwa kazi kubwa inaenda kufanywa na Serikali ili kufikisha asilimia 95 ya upatikanaji maji mijini na 85.

Aidha Dkt Adam O. Karia Mkuu wa Chuo cha maji amezishukuru Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya maji Kwa muitikio mkubwa na kujitokeza kushiriki Kongamano litakalokuja na na majibu sahihi ya changamoto za sekta ya maji na usafi wa mazingira.

Kongamano hili linaenda sambamba na utoaji elimu kwa umma juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi mbalimbali kupitia mabanda ya maonyesho yaliyopo katika kongamano hilo.

Previous articleSTAMICO YAUNGANA NA WANAWAKE DUNIANI KUSHEREHEKEA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI
Next articleRAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. SAMIA AKISALIMIANA NA WANANCHI WA BOMANG’OMBE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here