Home ENTERTAINMENTS CHRISTOPHER MWAHANGILA ATHIBITISHA KUSHIRIKI TAMASHA LA PASAKA

CHRISTOPHER MWAHANGILA ATHIBITISHA KUSHIRIKI TAMASHA LA PASAKA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Pasaka kila mwaka Alex Msama (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika bure bila kiingilio April 9, 2023 katika Viwanja vya Leders Club Jijini Dar es salaam.

Mratibu wa tamasha la Pasaka Bw. Emmanuel Mabisa (kulia) akifafanua jambo kuhusu maandalizi ya Tamasha hilo.

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Christopher Mwahangila (wa kwanza kushoto) akiiimba wimbo mbele ya waandishi wa habari kuonesha namna alivyojiandaa kutumbuiza kwenye Tamasha hilo. (katikati) ni, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha hilo kila mwaka Alex Msama, na (kulia) ni, Mratibu wa tamasha la Pasaka Bw. Emmanuel Mabisa.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Maandalizi ya Tamasha la Pasaka yamezidi kushika kasi ambapo mwimbaji mwingine wa nyimbo za Injli nchini Tanzania Christopher Mwahangila amethibitisha kushiriki kwenye tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Aprili 9, mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkuano na waandishi wa habari uliofanyika leo Machi 23,2023 katika Ofisi za Msama Promotion Kinondoni Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Alex Msama amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yanakwenda vizuri na kwamba waimbaji mablimbali wanaoshiriki kwenye tamasha hilo wameendelea kutambulishwa akiwemo Christopher Mwahangila aliyetambulishwa leo.

Aidha amesema kuwa tamasha hilo litakuwa la aina yake litakalowajumuisha watu wa Dini na Madhehebu yote na kwamba watu wote wanakaribishwa kwenye tamasha hilo.

“Kila Mtanzania anakaribishwa kupongeza jitihada zinazofanywa na Mama kwa kuwa alipokea nchi akiwa kwenye kipindi kigumu lakini bado tunafuraha, upendo na amani katika Taifa letu hivyo tamasha hili sio la kukosa, njooni tumpongeze mama kwa pamoja.” amesema Msama.

Kwa upande wake mwimbaji wa nyimbo za Injili Christopher Mwahangila ameahidi kutoa burudani safi na kukonga nyoyo za watanzania hususan wapenzi wa nyimbo za Injili ambapo amechukua fursa hiyo kuwakaribisha watu wote katika tamasha hilo.

“Tamasha la Pasaka litakonga nyoyo za waumini mbalimbali wa nyimbo za Injili na nitaimba live usipange kukosa, lakini pia tujitokeze katika kumpongeza Rais  Samia kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani ya miaka miwili,  njooni tusifu kwa pamoja.” amesema Mwahangila.

Naye mratibu wa tamasha la Pasaka Emmanuel Mabisa amesema kuwa maandalizi yote ya tamasha hilo yamekamailika huku akiwaomba watu wote kuwahi kwenye tamasha hilo ambapo vyakula na vinywaji vitapatikana viwanjani hapo kwa bei nafuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here