Home FASHIONS 7HILLS YA JITOSA KUDHAMINI MISS DAR ZONE 2023

7HILLS YA JITOSA KUDHAMINI MISS DAR ZONE 2023

NA: MWANDI WETU

MSIMU mpya wa shindano la Miss Dar es salaam, umezinduliwa rasmi jana katika hotel ya Onomo ambapo moja ya wadhamini wa mchuano huo ni kinywaji cha 7Hills.

Mchuano huo ambao utakutanisha warembo kutoka wilaya ya Temeke, Ilala, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo wata anza mchakato March 12, kwa kufanya usahili Onomo hotel Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar Es Salaam muwakilishi wa kinywaji cha 7Hills Fredy Kuja, amesema wamejikita kudhamini shindano hilo kwa sababu ni frusa kubwa kwa wasichana wenye ndoto katika tasnia ya urembo.

“Shindano la Miss Dar Zone, ni moja ya njia ya kuibua na kufikiaha wasichana wenye ndoto za kufanya vizuri kwenye tasnia ya mitindo na urembo ndio sababu ya sisi kukubali kungana na wandaaji ili kuhakikisha frusa hii ina fanikiwa kwa kiasi kikubwa,” Anasema Fredy Kuja.

Naye Muandaaji wa shindano hilo Linda Samsoni, amewataka warembo kujitokeza kwa wingi katika usahili huo ili kufikia ndoto zao.

“Niwakaribishe warembo wote wenye nia ya kushiriki mashindano ya Miss Tanzania, kujitokeza kwa wingi bila kuogopa kwa kuwa huu ndio mwanzo wa safari ya kufikia ndoto zao,” Anasema Linda Samsoni.

Aidha aliwashukuru wadhamini waliojitokeza kuwafadhili na kuomba tasisi na makampuni kuendelea kujitokeza kuwashika mkono ili kutimiza malengo ya wasichna wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here