Home LOCAL UWT ILALA YAWAKINGIA KIFUA BODABODA

UWT ILALA YAWAKINGIA KIFUA BODABODA

Na: Heri Shaaban (Ilala )

Umoja Wanawake (UWT )Wilaya Ilala imesema mgambo  wa halmashauri za manispaa wana kazi ya kulinda usalama wa nchi na raia lakini hawaruhusiwi kuigombanisha serikali na wananchi au kuwabughudhi bodaboda.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Umoja wanawake WIlaya ya Ilala UWT Neema Kiusa, katika Ziara zake na Kamati ya Utekekezaji kuangalia uhai wa jumuiya na kuwashukuru wanachama .

‘kazi ya Mgambo wa HALMASHAURI kulinda Usalama wa nchi na raia wake hawarusiwi kugombanisha Serikali na wananchi au mama lishe na wajasiriamali “alisema Neema .

Mwenyekiti Neema alisema UWT haifurahishwi na kukithiri na Vitendo vya manyanyaso vikifanywa na Baadhi ya Mgambo Ikiwemo kuwazuia bodaboda wasitoe huduma baadhi ya maeneo bila kutaja sababu za Msingi .

Alisema makundi ya bodaboda ,mama lishe na Wajasiriamali wadogo wanangaika kupata riziki zao halali hivyo si uungwana kuchukua pikipiki zao kuzilundika kituo Cha Polisi.

Aidha alisema UWT WIlaya ya Ilala imewataka Mgambo wa HALMASHAURI wanaokamata Bodaboda Wilayani Ilala kulinda Usalama wa raia na Mali zao bila kugombanisha Serikali na Wananchi ,bodadoda,mama lishe na wajasiriamali lazima wafanye kazi zao kwa uhuru .

Aliwataka Bodaboda na mama Lishe kufuata taratibu za HALMASHAURI bila bila kukiuka na kufuata taratibu za Usafi na kukabiliana na Vitendo vya wizi .

‘Mgambo mnapobeba samaki wa wafanyabiashara matunda l, mboga mboga au Bodaboda bila maelezo mnagombanisha Serikali na wananchi wakati Serikali yetu ni Sikivu elekezeni kwa taratibu bila kutumia nguvu”alisema .

Wakati huo huo Neema aliwataka Bodaboda kupuuza kauli ya Mbunge wa zamani wa Arusha Mjiji (CHADEMA) Godbless Lema anavyobeza kazi za Bodaboda na kuwaponda wakati bara Zima na Afrika na Asia kazi ya Bodaboda huendesha Maisha ya Watu .

Alisema UWT Ilala ina unga mkono vijana kujituma katika kazi ya Bodaboda kuliko vijana hao wakajiingiza katika vitendo vya uharifu wa kutumia silaha au utapeli..

Mwisho
Heri Shaaban.
Habari 0714872471
0755872471

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here