Home LOCAL RAIS SAMIA AHUTUBIA LATILA BARAZA LA WANAWAKE LA WANAWAKE CHADEMA, MOSHI KILIMANJARO

RAIS SAMIA AHUTUBIA LATILA BARAZA LA WANAWAKE LA WANAWAKE CHADEMA, MOSHI KILIMANJARO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Maridhiano kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe aliyeikabidhi kwa niaba ya Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) mara baada ya kuwahutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023.
Viongozi mbalimbali wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) pamoja na Wanachama wa Chama hicho wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia katika Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) pamoja na Wanachama wa Chama hicho kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe, pamoja na viongozi mbalimbali wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) mara baada ya kuwahutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here