Home Uncategorized YANGA SC YAONGEZA KASI YA UBINGWA

YANGA SC YAONGEZA KASI YA UBINGWA

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Yanga SC imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo kwa kuendeleza ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC katika mchezo uliopigwa kwenye Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Goli la Yanga lilipachikwa kambani na mshambuliaji wake Clement Mzinze katika dakika ya 38 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo lililodumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo katika dakika ya 75 Yanga ilifanya mabadiliko kwa kumpumzisha Clement Mzinze na kumwingiza Fiston Mayele huku Mudathir Yahaya akiingia kuchukua nafasi ya Zawadi Mauya.

Hadi mwamuzi wa mchezo huo anapuliza kipyenga cha mwisho, timu ya Yanga imetoka kifua mbele kwa kuchukua alama 3.

Baada ya Matokeo hayo Yanga inafikisha alama 62 ikitofautiana na Simba SC kwa jumla ya alama 8 hivyo kuwafanya Yanga kuendelea kushika usukani wa msimamo wa Ligi hoyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here