Takriban watu 1,900 wanaaminika kufariki baada ya matetemeko mawili ya ardhi kupiga Uturuki na Syria.
Idadi ya waliothibitishwa kufariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea asubuhi ya leo nchini Uturuki sasa imefikia 1,121, mkuu wa Mamlaka ya kudhibiti Maafa na Dharura nchini humo
Idadi ya waliouawa nchini Syria sasa imefikia 783, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, ambalo limekuwa likijumuisha takwimu kutoka kwenye mamlaka katika maeneo yanayoshikiliwa na serikali na wale wa kundi la uokoaji la The White Helmets katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi.
Takwimu zinaleta jumla ya pamoja kuwa takribabi 1,797.
Taarifa bado zinaibuka kuhusu athari za tetemeko la pili lililokumba mkoa wa Kahramanmaras nchini Uturuki saa chache baada ya lile la kwanza kutokea karibu na mji wa Gaziantep, karibu maili 80 kusini.
Watu wapatao 70 walikuwa tayari wamethibitishwa kuuawa huko Kahramanmaras kabla ya tetemeko la pili kupiga.
Idadi ya waliofariki sasa inatarajiwa kuongezeka huku juhudi za kuwaokoa zikiendelea.