Home BUSINESS USHUSHWAJI WA MELI YA MV MWANZA MAJINI UTASAIDIA KUKUZA SEKTA YA UTALII

USHUSHWAJI WA MELI YA MV MWANZA MAJINI UTASAIDIA KUKUZA SEKTA YA UTALII

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema zoezi la ushushwaji wa Meli ya MV Mwanza “HAPA KAZI TU” kwenye maji, itasaidia kukuza utalii katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nchi za jirani.

Ameyasema hayo leo Februari 12,2023 wakati wa hafla ya ushushaji meli ya MV Mwanza “HAPA KAZI TU” majini katika Bandari ya Mwanza Kusini.

“Utalii wa Kanda ya Ziwa unaenda kufunguka kupitia tukio hili na pia Meli hii itakuwa inazunguka katika nchi za jirani ikiwemo Kenya na Uganda hivyo zitaweza kufaidika na masuala ya shughuli za utalii” Mhe. Masanja amesisitiza.

Ameongeza kuwa kupitia tukio hilo la ushushwaji wa meli kwenye maji unaenda kuongeza zao jipya la utalii na kutakuwa na utalii wa meli.

Aidha, Mhe. Masanja amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha jiji la Mwanza na Mikoa ya Jirani ya Kanda ya ziwa inaenda kufaidika kwa asilimia kubwa na miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa meli ya MV Mwanza “HAPA KAZI TU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here