Lilian Mugwe Afisa maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala ya kijinsia katika halmashauri hiyo.
Bi. Khadija John ambaye pia ni mnufaika na mkai wa Nyamuswa wilayani Bunda akichangia maoni yake kuhusu masuala kijinsia katika wilaya ya Bunda.
Bi. Nyagige Bisendo ambaye ni mnufaika wa TASAF katika Halmashauri hiyo kutoka eneo la Nyamuswa Bunda akitoa maoni yake eneo la Nyamuswa wilayani Bunda.
Bi. Faraja Luhanjo kutoka Dawati laMalalamiko TASAF akizungumzana walengwa wa TASAF na kuwapa maelekezo namna ya kuwasilisha malalamiko yaowakati wanapopata changamoto.
Mpango wa Kunusuru kaya za Walengwa ,wa TASAF umehamasisha pakubwa wanawake katika Halmashauri ya wilaya ya Bunda kujitambua na kuondokana na unyanyasaji wa kijinsia ambao walikuwa wakiupitiakatika jamii,.
Wanawake wengi wamehamasika kupeleka watoto wao shule, Kliniki, Kupanga mipango ya familia pamoja na masuala mbalimbali ikiwemo kushiriki katika masuala ya uongozi na vikao vya maamuzi mbalimbali katika jamii zao.
TASAF pia imesaidiwa wanawake kuwapa watoto wao lishe bora na wengi wao kujiamini hivyo kushiriki mambo muhimu kwa kujiingaza katika vikundi mbalimbali vya kijamii na kuwawezesha kuchangia maendeleo katika familia zao.
Hayo yameelezwa na Lilian Mugwe Afisa maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika wilayani humo ili kuona shughuli mbalimbali zinazofanya na TASAF ambapo ameongeza kwamba wanawake wengi wanapokuwa na uwezo wa kipato wanaheshimika katika jamii zao.
Mpango huo pia umesaidia kupunguza unyanyasaji wa Kijinsia kwani wanawake hao wamekuwa na uwezo wa kujitafutia mahitaji yao kwa kufanya Biashara ndogo ndogo na kuepuka kuwa tegemezi kwa kuendesha mambo yao na familia kwa ujumla wake.
Aidha Lilian ameongeza kwamba kutokana na mafunzo wanayopata kupitia TASAF imewasaidia kujiamiani na hata wengine kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbali mbali za uongozi.
Hata hivyo bado hawana nguvu kwa kiasi kikubwa kwa sababu katika jamii yetu wanaume wamekuwa hawaamini kwamba mwanamke anaweza kuongoza jambo ambalo kwa kiasi fulani limekuwa likiwakwamisha wanawake.