Home BUSINESS TASAC YATOA SEMINA ELEKEZI KWA KAMATI YA BUNGE YA PIC DODOMA

TASAC YATOA SEMINA ELEKEZI KWA KAMATI YA BUNGE YA PIC DODOMA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge akifafanua jambo kwa Kamati ya PIC wakati wa Semina Elekezi kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya PIC iliyofanyika Februari 8, 2023 Jijini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge alipokua akitoa mada katika semina hiyo, Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge (wa kwanza kulia) akisalimia na mjumbe wa kamati ya PIC mara baada ya kumalizika kwa Semina hiyo, Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge (kulia) akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PIC Mhe. George Malima (Mb) mara baada ya kumaliza Semina Elekezi kwa Kamati hiyo jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC Nah. Mussa H. Mandia (kushoto) akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PIC Mhe. George Malima (Mb) mara baada ya kumaliza Semina Elekezi kwa Kamati hiyo jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA TASAC)

Na: Mwandishi TASAC

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limefanya semina elekezi kwa Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) jijini Dodoma tarehe 8 Februari, 2023.

Semina hiyo ililenga kutoa uelewa kwa Kamati hiyo kuhusu majukumu yanayotekelezwa na TASAC, miradi inayosimamiwa na Shirika, Mpango Mkakati wa Shirika, mafanikio, fursa pamoja na changamoto zinazolikabili Shirika na Sekta ya Usafiri Majini nchini.

Katika Semina hiyo, wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Makamu Mwenyekiti Mhe. George Malima (MB), waliishukuru TASAC kwa kutoa semina hiyo ambayo imejibu na kuleta uelewa wa masuala mbalimbali ambayo yatawapa urahisi katika utendaji kazi wa kila siku kwenye Kamati hiyo na pia kuishauri Serikali kuhusu Sekta ya Usafiri Majini.

Previous articleRAIS SAMIA AMTEUA BALOZI EPHRAIM MAFURU ATEULIWA KUWA MTENDAJI MKUU AICC
Next articleWAZIRI MKUU AZINDUA NYARAKA ZA USIMAMIZI WA MAAFA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here