Home BUSINESS TANZANIA KUANZA SAFARI ZA NDEGE MOJA KWA MOJA HADI SAUDI ARABIA

TANZANIA KUANZA SAFARI ZA NDEGE MOJA KWA MOJA HADI SAUDI ARABIA

Tanzania inategemea kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja hadi Saudi Arabia ambapo safari ya kwanza kati ya Dar es Salaam na Jeddah inatarajiwa kuanza tarehe 26 Machi 2023.

Hayo yamebainishwa katika mazungumzo ya Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Alabdulwahab na kujadili maandalizi ya uzinduzi wa safari za ndege za moja kwa moja kati ya Tanzania na Saudi Arabia.

Katika mazungumzo yao viongozi hao pia walijadili mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za Tanzania hususan nyama na matunda.

Previous articleNMB YAPATA UFADHILI WA BILIONI 572 KUTOKA JUMUIYA YA ULAYA
Next articleTANZANIA NA BANKI YA DUNIA ZASAINI MKOPO NAFUU WA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here