Home Uncategorized SIMBA SC YACHEZEA KICHAPO 3-0 NA RAJA CASABLANCA

SIMBA SC YACHEZEA KICHAPO 3-0 NA RAJA CASABLANCA

Timu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC imezamishwa kwa kupokea kichapo cha  mabao 3-0  na timu ya Raja Casablanca ya nchini Morocco mchezo uliopigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo  huo wa Kundi C wageni Raja Casblanca ilionesha kandanda safi huku wakilishambulia lango la Simba. 

Katika dakika ya 30 ya mchezo huo Raja Casablanca ilipata goli lake la kupitia kwa  na Hamza Khabba baada ya kuwazidi maarifa mabeki na viungo wa Simba na kuachia shuti kali lililomshindwa Mlinda mlango wa Simba SC Aishi Manula.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo wageni walifaidika na mabadiliko hayo kwani waliweza kupata mabao mawili  kupitia kwa Benjdid dakika ya 80 na 

Kwa ushindi huo Raja Casablanca imeweka rekodi ya kupata Pointi tatu katika uwanja wa Taifa kwani Simba tangu 2013 haijawahi kufungwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwa matokeo hayo Kundi C Raja Casabblanca amefikisha Pointi 6,nafasi ya pili Horoya wenye Pointi 4,Vipers pointi 1 wakiwa nafasi ya tatu huku Simba akishika nafasi ya nne akiwa hana pointi wala bao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here