Home Uncategorized MKE NA MME WANASHIKILIWA NA POLISI TUHUMA MAUAJI YA MAMA YAO.

MKE NA MME WANASHIKILIWA NA POLISI TUHUMA MAUAJI YA MAMA YAO.

Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa tuhuma ya kumuua kwa kumchinja Mwanamke Mmoja alietambulika kwa jina la Butamo Igonzele(70) Mkazi wa kijiji cha Bumegezi jata ya Ihanamilo wilaya ya Geita Mkoani Geota.

Jeshi hilo linawashikiria Joyce Julius ambaye ni mtoto wake na Marehemu na Juma Charles ambaye ni Mkwe wa Marehemu ambao inadaiwa walikuwa wanamtuhumu Marehemu kuhusika na kifo cha mtoto wao ambaye alifariki wiki Moja iliyopita.

Tukio hilo limetokea Februari 23, 2023 majira ya usiku katika Kijiji hicho cha Bunegezi Kata ya Ihanamilo Wilaya ya Geita Mkoani humo ambapo watuhumiwa hao wanadaiwa kumuua Mama yao.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Polisi Berthaneema Mlay amesema watu hao wanashikiriwa na Jeshi hilo kwa ajiri ya upelelezi wa kina ili kubaini wahusika.

“Bibi huyu alikatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kupoteza maisha kwa kuvuja damu nyingi; mwili wake umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Geita,” amesema kaimu Kamanda.

watuhumiwa hao wamemakatwa baada ya uchunguzi wa awali kuonyesha wanaweza kuhusika katika mauaji hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here