Home Uncategorized MAMA MJAMZITO AUWAWA NA MAJAMBAZI, NAO WAUWAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI

MAMA MJAMZITO AUWAWA NA MAJAMBAZI, NAO WAUWAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI

NA. COSTANTINE JAMES, GEITA.

Watu watatu akiwemo mama mjamzito wameuwawa katika kitongoji cha kilimahewa kata ya Ludete katika mji mdogo wa Katoro uliopo wilayani Geita Mkoani Geita huku wawili wakisadikiwa kuwa ni majambazi baada ya kuvamia usiku katika familia ya Msafiri Renatusi.

Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usku ambapo mama huyo mjamzito alietambulika kwa jina la Elinata Elias (27) ameuwawa kwa kuchinjwa shingo na kitu chenye ncha kali huku baba wa familia hiyo Msafiri Renatus akijeruhiwa vibaya.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema majambazi hao akiwemo mtoto wa kiume wa Msafiri Renatus alietambulika kwa jina la Jackson Msafiri (25) akiwa na rafiki ambaye jina lake halijafahamika walifika katika familia hiyo na kutekeleza mauaji ya mama huyo.

Baada ya kutekeleza maauji hayo majambazi hao waliuwawa na wananchi wenye hasira kali ambao walikuwa wamezingira nyumba hiyo na baada ya kutekeleza tukio hilo walishindwa kutoroka hali iliyopelekea kuwawa na wananchi waliokuwa na siraha za jadi.

Mwenyekiti wa kitongoji cha kilima hewa Michael Chuma pamoja na msemaji wa Familia Mihayo Renatus wamesema chanzo cha kijana huyo kutekeleza mauajia hayo pamoja na Rafiki yake ni tamaa za mali ya Baba yake baada ya kuachana na mama yake kisha kuoa mwanamke mwingine.

Mganga mfawidhi wa kituo cha afya katoro Dkt. Zakayo Sungura amethibitisha kupokea miili ya watu hao watatu pamoja na Baba wa Familia hiyo Msafiri Renatus (40) ambae alikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita kwa ajiri ya matibabu zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here