Home LOCAL HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM YAPITISHA BAJETI SH. BILIONI 90

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM YAPITISHA BAJETI SH. BILIONI 90

Na:  Heri Shaaban (Ilala )

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imepitisha Bajeti ya shilingi Bilioni 90 kwa mwaka wa fedha 2023 /2024.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2324 vipaumbele vya Halmashauri Barabara na Miundombinu ambapo Halmashauri hiyo imetenga shilingi bilioni 15 wameelekeza katika Barabara .

“Halmashauri yetu ya Jiji na Baraza langu la madiwani wa Jiji Leo tumepitisha bajeti ya shilingi milioni 90 katika pesa hiyo tumeweka kipaumbele BARABARA za ndani zote shilingi milioni 15 pesa zingine zimeelekezwa katika huduma za Jamii “ alisema Kumbilamoto .

Meya Kumbilamoto alisema Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde alifanya ziara katika Wilaya hiyo ameona changamoto mbalimbali Pugu na Kituo cha Afya Buyuni hivyo pesa zimeelekezwa katika Bajeti hii ya 2023 kutatua kero .

Aidha alisema bajeti hiyo pia ya mwaka huu imegusa miradi mikubwa ya Serikali ambayo itajengwa Kata ya Mchafukoge sehemu ya kuegesha magari ,soko la kisasa Ilala na mradi mkubwa wa kituo cha Afya Mchikichini .

Aliwapongeza madiwani kwa pamoja kupitisha bajeti hiyo ikiwemo Kamati ya Huchumi na Huduma za Jamii na Kamati ya Mipango Miji ambapo watajenga magolofa mawili ya Sekondari na mikopo ya asilimia 10 wametenga bajeti kwa ajili ya Wanawake ,Vijana na Watu wenye ulemavu

Meya Kumbilamoto aliwataka Watendaji wa Halmashauri ya Jiji Sasa kuchapa kazi na kusimamia miradi ya Maendeleo ya Serikali ya awamu ya sita ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameelekeza wilayani Ilala Kwa ajili ya utekekezaji wa Ilani .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here