Home Uncategorized GRANDI APONGEZA UREJEAJI WA WAKIMBIZI WA BURUNDI NA KUHIMIZA MISAADA ZAIDI

GRANDI APONGEZA UREJEAJI WA WAKIMBIZI WA BURUNDI NA KUHIMIZA MISAADA ZAIDI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi (UNHCR) Bw. Filippo Grandi aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi (UNHCR) Bw. Filippo Grandi na Ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi (UNHCR) Bw. Filippo Grandi ambaye aliambatana na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.

Bujumbura (Burundi) na Dodoma (Tanzania), 10 February 2023

Wakati hali ya Burundi inaendelea kuimarikaKamishnaMkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi, Filippo Grandiamesisitiza dhamira ya UNHCR ya kusaidia wakimbizi kurejea salama kutoka katika nchiwalizopewa hifadhi.

Tangu mwaka 2017, zaidi ya wakimbizi 200,000 wa Burundi wamesaidiwa na UNHCR kurejea nchini kwao kwa hiarikutoka nchi jirani ikiwemo Tanzania.

Akihitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Burundi, Grandiamemshukuru Rais Evariste Ndayishimiye kwa juhudi za kuleta utulivu nchini Burundi.  

Tunaishi katika ulimwengu wenye fursa chache tu za kuwezakusaidia kutafuta suluhisho la kudumu kwa wale wanaolazimika kuyakimbia makazi yao.

Mara nyingimigogoro hudumu kwa muda mrefu lakini ninafarijika kuonawakimbizi wa Burundi wanafanya uamuzi wa kurejeanyumbani baada ya miaka mingi uhamishoniSote tunapaswakufanya kazi ili kuhakikisha wanapata suluhisho la kudumu,” alisema Grandi.

Juhudi za Serikali ya Burundi na wadaukatika kusaidia wakimbizi wa Burundi wanaorejea nyumbanizinatia moyo sana.”

Grandi ametembelea eneo la Rugombo na kuonana na baadhiya wakimbizi ambao wamerejea nyumbani hivi karibuni na kushuhudia misaada inayotolewa na UNHCR na wadau ilikuwawezesha kujenga upya maisha yao.  

Misaadainajumuisha usafirichakulafedha taslimu, na vifaa vya nyumbani kwa wakimbizi wanaorejea Burundi.

Kwa kuzingatia ukubwa wa mahitaji, UNHCR imeamua kuboreshana kuimarisha misaada kwa wanaorejea.

“Hata hivyotunahitaji wadau wa maendeleo kusaidia kuboresha upatikanaji wa huduma, na shughuli za kijamiikwa wakimbizi wanaorejeaHawa ni raia wa Burundi na wanahitaji kujumuishwa katika mipango ya maendeleo Grandi aliongeza.

Burundi pia inahifadhi wakimbizi 80,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Grandi ametembelea kituocha wakimbizi cha Cishemere kilichopo Kaskazini Magharibimwa nchi na katika eneo linalopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kukutana na wakimbizi wanaokimbia machafuko na ukatili Mashariki mwa DRC

Grandi amewasili mkoani Dodoma leo akitokea Burundi na kufany.a mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan.

Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa, ni hatua za mafanikiozinazoendelea kutekelezwa katika kuboresha mazingira na mahitaji nchini Burundi kwa wale wanaoendelea kurejea.

Grandi pia ameshukuru utamaduni wa muda mrefu wa Tanzania wa kukaribisha wakimbizi na juhudi zinazoendeleaza kuwahudumia wale wanaokimbia migogoro na mateso.

Kwa takwimu, Tanzania inahifadhi idadi kubwa ya wakimbizi wa Burundi dunianiTakribani wakimbizi na waomba hifadhi248,000 wengi wao kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaishi Tanzania.

Shirika litaendelea kufanya kazi kwa karibu na SerikaliMashirika,na wafadhili, pamoja na wadau wa maendeleoilikuhifadhi na kutafuta suluhisho kwa wale wanaolazimika kuyakimbia makazi yao.” alisema Grandi. 

Katika muktadha huoUNHCR inapokea kwa furaha tangazola Umoja wa Ulaya la kutoa ufadhili wa Euro milioni 40 katika miaka ijayo kwa washirika wanaosaidia kuboreshamazingira ya urejeaji nchini Burundi.

Ufadhili huoutawanufaisha wakimbizi wa Burundi katika ukanda huu, pamoja na wale waliorejea nyumbanikwa kuhakikishawanapata usaidizi wanaohitaji ili kuishi kwa usalama na heshima.

Ufadhili huo utajumuisha ulinzi na uthabitimsaadawa kisheriamasuala ya ukatili wa kijinsiaujuzi wa kusomana kuandika na shughuli za kilimo

Previous articleATAKAYEMZUIA MWANAFUNZI KUPATA ELIMU KUCHUKULIWA HATUA-MAJALIWA
Next articleWATAALAM WA JKCI WAADHIMISHA SIKU YA WAPENDANAO KWA KUFANYA UPASUAJI KWA WATOTO 15
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here