Home LOCAL DKT. TAX ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA UTURUKI

DKT. TAX ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA UTURUKI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Uturuki Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Uturuki Jijini Dar es Salaam, kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Uturuki tarehe 6 Februari, 2023.

Baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Dkt. Tax ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Uturuki na kuwasihi kuendelea kuwa wavumilivu wakati huu wa msiba mkubwa kwa Taifa hilo uliosabaisha vifo vya watu zaidi ya 18,000.

“Serikali ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla tunaungana na Serikali ya Uturuki katika kuombeleza msiba huo mzito,” alisema Dkt. Tax.

Mwaka 1999 Uturuki ilikumbwa na tetemeko la ardhi ambapo watu wapatao 17,000 walipoteza maisha kutokana na tetemeko hilo. Kadhalika, mwaka 2011 ilikumbwa na tetemeko la ardhi katika mji wa Van lilipelekea vifo vya watu 500.

Previous articleBOT YASHINDA TUZO YA UZINGATIAJI SHERIA, KANUNI ZA SERIKALI MTANDAO
Next articleATAKAYEMZUIA MWANAFUNZI KUPATA ELIMU KUCHUKULIWA HATUA-MAJALIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here