Jaji Mfawidhi wa Mahakama Mkuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Jaji. Paul Joel Ngwembe ameitaka jamii kutambua kuwa upelelezi na uendeshaji wa kesi zinazohusu makosa ya kijinai ni wa kisayansi zaidi kuliko hisia na nadharia za kizamani kama wengi wanavyo dhani.
Jaji Ngwembe amesema hayo Febreary 27 mkoani Morogoro wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa Waendesha mashtaka na wapelelezi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini yaliyoandaliwa na Mhakama ya Tanzania na kuendeshwa na Chuo cha Ungozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa ufadhili wa banki ya Duania kupitia mradi wa maboresho awamu ya pili.
Alisema Makosa mengi yanathibitishwa kisayansi kwa kutumia DNA, Vipimo vya Kidaktari kwa kutumia wataalam wa utambuzi wa maandishi hivyo haki jinai haiwezi kupatikana bila kuhakikisha kuna wapelelezi wenye ujuzi na weledi usio tia shaka na walio tayari kutumia ujuzi huo kuhakikisha wale tu wanao tuhumiwa kufanya makosa wanafikishwa Mahakamani na Haki yao wanaipata.
“Siridhishwi na makosa mengi yanayofikishwa mahakamani bila kuwa na upelelezi ulio kamilika, au kumkamata mtuhumiwa na kumshikilia kwenye vituo vya polisi bila kuwepo kwa upelelezi wa dhati unao mhusisha mtuhumiwa. ”alisema.
“Makosa yenye adhabu ya vifungo vya Muda mrefu, kama ubakaji, ulawiti mahusiano yaliyo haramishwa kwa sheria yaani incest by male wakati mwingine yametumika kudhalilisha watu wasio na hatia, hata ugomvi wa Kifamilia hupelekea kuhusisha makosa ya namna hiyo.”aliongeza.
Alisema mahakama imejiwekeamalengo ya kumaliza Mashauri kikamilifu na upatikanaji wa haki kwa wakati ili kuongeza imani ya wananchi kwa mahakama, lakini pia vyombo vya haki jinai na hivyo kuwepo kwa misingi bora ya amani na utulivu.
“Siridhishwi na makosa mengi yanayofikishwa mahakamani bila kuwa na upelelezi ulio kamilika au kumkamata mtuhumiwa na kumshikilia kwenye vituo vya polisi bila kuwepo kwa upelelezi wa dhati unao mhusisha mtuhumiwa.” Alisema Jaji Paul Ngwembe.
Awali Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama kuu Arnold Kirekiano alisema mafunzio hayo ya siku tato yanalenga kupunguza na kumaliza mashauri ya mlundikano yaliyopo mahakanai yanayochelewa kusikilizwa kutokana na upelelezi kutokamilika kwa wakati ifikapo mwaka 2025.
Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maboresho ya mahakama ambayo yanatekelezwa kupitia mpango makakati wa miaka mitano mwaka 2020- 2025pia nisehemu ya utekelezaji sera ya mafunzo ya Taifa 2003 pamoja na sera ya mafunzo ya Kimahakama 2019.
Mafunzo hayo yamehusisha taasisi saba ambazo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori na Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu.