Home BUSINESS BOT YASHINDA TUZO YA UZINGATIAJI SHERIA, KANUNI ZA SERIKALI MTANDAO

BOT YASHINDA TUZO YA UZINGATIAJI SHERIA, KANUNI ZA SERIKALI MTANDAO

Benki Kuu ya Tanzania imeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha ‘Uzingatiaji wa Sheria, Miongozo na Kanuni za Serikali Mtandao’.

Tuzo hiyo kwa BOT imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma, Mhe. Deogratius Ndejembi, tarehe 8 Februari 2023 jijini Arusha kwenye kikao kazi cha 3 cha Serikali Mtandao kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).

Kikao kazi hicho kimewakutanisha watumishi wa umma na wadau wengine kutoka taasisi mbalimbali za Serikali kujadili juu ya mafaniko na changamoto za utekelezaji wa serikali mtandao (matumizi ya TEHAMA serikalini) kikiwa na kauli mbiu ya “Mifumo Jumuishi ya TEHAMA kwa utoaji bora wa huduma za umma”.

Aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ni Meneja Idara ya Uundaji na Usimamizi wa Mifumo, Bw. Christopher Nyato.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here