Home Uncategorized POLISI MKOA WA ILALA YAPIGA VITA VITENDO VYA UKATILI 

POLISI MKOA WA ILALA YAPIGA VITA VITENDO VYA UKATILI 

Na: Heri Shaaban (Ilala)

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala limepiga marufuku vitendo vya ukatili kwa wanafunzi Wilaya ya Ilala badala yake Wanafunzi wametakiwa kuzingatia masomo .

Tamko hilo limetolewa Dar es Salaam jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Debora Magilimba alipokuwa akitoa Elimu ya kupinga vitendo vya ukatili kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Pugu .

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala linapinga vitendo vya ukatili kwa wanafunzi wa shule za Wilaya ya Ilala tunaomba Wanafunzi mzingatie masomo na kufuata nidhamu za shule Ili kukuza taaluma shuleni “ alisema Debora .

Kamanda Debora aliwataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya pugu wawe na nidhamu na kufuata taratibu za Walimu na Wazazi wawapo shuleni waache tabia ya kutoroka Shule .

Aliwataka Wakuu wa shule kufatilia kwa Karibu mienenendo Wanafunzi wao na kiwatolea taarifa wachukuliwe hatua.

Wakati huo huo Kamanda Debora alipiga marufuku Wanafunzi kutumia simu ya mkononi wawapo shuleni badala yake Wanafunzi wametakiwa kujitambua na kuzingatia masomo yao wakiwa Darasani Ili kukuza taaluma .

Mkuu wa shule ya Sekondari Pugu Juma Orenda alisema shule ya Sekondari ya Pugu imeanzishwa Mwaka 1948 ilikuwa ikiitwa St’Fransisi Mwalimu Julius Nyerere alijiunga shule hiyo akiwa Mwalimu wa Kiswahili mpaka mwaka 1954 akaenda kujiunga na Siasa ,mwaka 1954 kulikuwa na Wanafunzi mbalimbali Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda na hayati Benjamini Mkapa walisoma shule hiyo .

Mkuu Juma Orenda alisema kwa Sasa shule ya Pugu ina jumla ya Wanafunzi 959 wa mahitaji Maalum 108 idadi ya Walimu 71 kati yao wa kike 44 Wanaume 27.

Akizungumzia taaluma ya shule alisema kidato cha pili Pugu Sekondari asilimia 99 wote wamefaulu ,Wanafunzi wa kidato cha nne 143 wote wamefaulu asilimia 100 na mwaka 2022 Wanafunzi 129 walifanya mtihani kati yao watano wamefeli .

“Sekondari ya Pugu ni shule kubwa Tanzania kitaaluma ni shule kongwe mikakati ya Shule yetu kufanya Vizuri kitaaluma changamoto wanafunzi nidhamu “ alisema Juma .

Mrakibu wa Magereza Gereza Kuu la Ukonga SP, Juliana Daffi aliwataka wazingatie masomo darasani na kuwa walinzi wa kila mtu na aliwaasa waache vitendo vya ukatili vikitokea vitendo vya ukatili watoe taarifa katika uongozi wa SHULE .

SP Juliana Daffi alisema uhalifu unanzia ngazi ya chini amewataka wazazi wawalinde watoto hali mbaya Jamii inatakiwa kujua tunapoelimisha Wanafunzi na Jamii nyingine.

Katibu Tawala Wilaya ya Ilala Charangwa Selemani alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ilala imepokea changamoto za Shule hiyo wakashuka kuongea na wanafunzi na kutoa elimu.

Mwisho
HERI SHAABAN
Mwandishi wa habari
0714 872471
0755 872471

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here